The House of Favourite Newspapers

Dodoma wamsubiri Bella kwa hamu Julai 22

0

BELLAStori: Boniphace Ngumije

KWA mara ya kwanza King of The Best Melodies, Christian Bella ‘Obama’ anatarajiwa kupiga bonge ya shoo ya kihistoria Julai 22, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Royal Village, Dodoma.

Akizungumza na Uwazi, mratibu wa shoo hiyo, Renatus Gregory alisema kuwa usiku huo Bella atapiga nyimbo zake zote kali kuanzia Yako Wapi Mapenzi, Safari Siyo Kifo, Nashindwa, Amerudi, Nani Kama Mama na nyingine kibao.

“Usiku huo pia kutakuwa na DVD za miaka 10 ya Bella tangu aingie kwenye muziki. Mashabiki waje kwa wingi waone shoo ya live kwa kutumia vyombo kutoka kwa mkali wa masauti,” alisema Renatus huku akiongeza kuwa, usiku huo kiingilio kitakuwa shilingi 30,000 kwa VIP na kawaida shilingi 10,000.

Kwa upande wa wakazi wa Dodoma waliobahatika kuzungumza na gazeti hili walisema wanamsubiri mkali huyo wa masauti kwa hamu maana usiku huo utakuwa hautoshi.

Leave A Reply