The House of Favourite Newspapers

Shigongo awahimiza wanafunzi Muhimbili kuwa wabunifu

0

10 Na Hilaly Daudi

MKURUGENZI Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers, Eric  Shigongo Jumamosi iliyopita alihutubia  wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Udaktari Muhimbili ambao wameunda umoja wao unaojulikana kama Muhimbili University Fellowship of Evangelical Students na kusema kuwa taaluma wanayoichukua ni nzuri lakini akawashauri kuwa wabunifu ili wajiongezee vipaji vingine ili kujiongozea mapato.

18Shigongo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika kikundi hicho ambacho kilifanya mkutano wake katika ukumbi uliopo chuoni hapo ujulikanao kwa jina la Muhimbili Lecture Theatre 5, aliwahimiza wanachuo hao kuwa na ubunifu mkubwa ili kuweza kufanikiwa katika maisha.

11“Wito wangu ni kwamba muwe na vyanzo vingi vya mapato katika maisha yenu kwani kutawafanya mjiongezee  nafasi kubwa ya kukuza uchumi na kuleta maendeleo ndani ya familia zenu,” alisema Shigongo.

Pia aliwahimiza wanafunzi hao kutokata tamaa katika maisha yao hata kama watakuwa wanakutana na vikwazo vingi kwani hayo ni madaraja tu ya mapito ili waweze kufanikiwa.

Leave A Reply