The House of Favourite Newspapers

DOGO JANJA AKOSHWA NA CAROL NDOSI

KATIKA kuisindikiza Siku ya Wanawake Duniani, iliyofanyika juzi (Alhamisi), mkali wa michano Bongo, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’, amefunguka kwamba, kwa upande wake mwanamke ambaye amemkosha kwa mwaka huu ni mjasiriamali, Carol Ndosi.

 

Akipiga stori na Mikito Nusu Nusu, Dogo Janja alisema, Carol amemvutia kutokana na namna anavyojituma hata kuiingizia serikali pato la taifa.

 

“Carol kiukweli ‘ananiinsipaya’ sana. Ni mwanamke shujaa kwangu kwa mwaka huu. Tazama matamasha yake aliyokuwa anaandaa kama vile la Nyama Choma Festival. Unaona kabisa ni mbunifu na kupitia matamasha hayo ameweza kuliingizia taifa pato kubwa!” Alimaliza Dogo Janja

 

Stori: Boniphace Ngumije

Comments are closed.