The House of Favourite Newspapers

Donald Trump Aja na Madai Mazito Dhidi ya FBI, Alaani Jitihada za Kumdhoofisha Kisiasa

0
FBI wamefanya msako makali kwenye makazi ya Donald Trump

WIKI iliyopita, Maafisa wa Usalama Marekani (FBI) walivamia katika nyumba ya aliyekuwa Raisi wa marekani Donald Trump na kusema walipata nyaraka za “siri kuu” kutoka katika nyumba hiyo, zikiwemo baadhi zilizokuwa na taarifa ambazo zinaweza kusababisha uharibifu mkubwa  kwa maslahi ya Marekani ikiwa itafichuliwa hadharani.

 

Trump alielezea tukio hilo kama shambulio la kisiasa kutoka kwa wapinzani, Rais huyo wa zamani wa Marekani alidai Maafisa wa FBI waliiba hati zake tatu za kusafiria wakati wa uvamizi wa nyumba yake ya Mar-a-Logo.

 

Katika chapisho kwenye mitandao ya kijamii, Trump aliwaambia wafuasi wake “Katika uvamizi wa FBI wa Mar-a-Lago, waliiba hati zangu tatu (moja ilikwisha muda wake), pamoja na kila kitu kingine. “Hili ni shambulio la kisiasa katika kiwango ambacho hakijawahi kuonekana katika nchi yetu”

Trump amelaani vitendo vya FBI kuwa ni mpango wa kumdhoofisha kisiasa

Afisa wa Idara ya Haki alitoa majibu kwamba pasipoti za Trump tayari zimerejeshwa kwa Rais huyo wa zamani wa Marekani.

 

Wafuasi wa Trump kwa kiasi kikubwa wamechoshwa na msako huo, huku wakikosoa hatua hiyo kuwa ya kisiasa kutokana kwamba inafanyika wakati ambapo wengi wanatarajia atangaze mipango ya kugombea muhula mwingine wa Uraisi.

 

Imeandikwa: John Mbwambo kwa msaada wa mitandao

Leave A Reply