Donny Van De Beek Aomba Tena Kuondoka United

STAA wa Manchester United, Donny van de Beek anataka kuhakikisha tena anapeleka ombi la kuondoka kwenye timu hiyo katika usajili wa Januari. Beek amekuwa hana nafasi kwenye kikosi cha United kuanzia alipojiunga nao akitokea Ajax ya nchini Uholanzi.

 

Wachambuzi wengi wa soka walipinga kitendo cha mchezaji huyo kusajiliwa na United kwa kuwa waliona kuwa ana nafasi finyu sana ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza.

 

Inaelezwa kuwa mchezaji huyo alikasirika baada ya kuendelea kukaa nje kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Villarreal.

 

Taarifa kutoka kwenye mazoezi ya Man United inasema kuwa kiungo huyo alimuomba kocha wa timu hiyo kama inawezekana auzwe kwenye usajili wa Januari mwakani.

 

Amekuwa akisema kuwa kama akikosa nafasi hivyo mara kwa mara basi hataweza kucheza kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Uholanzi. Beek amefanikiwa kuanza kwenye michezo miwili tu msimu huu ya Kombe la Carabao.

MANCHESTER, England


Toa comment