The House of Favourite Newspapers

Dorah Asimulia Alivyonyanyaswa Kisa Umbo Lake -Video

0

MUIGIZAJI Wansekula Zacharia ‘Dorah’, amesimulia jinsi ambavyo jamii ilikuwa ikimyanyapaa kabla hajawa maarufu kutokana na kuwa na umbile dogo.

 

Dorah aliyasema hayo jana alipokuwa akifanya mahojiano na Kipindi cha HotPot kinachorushwa live kupitia +255GlobalRadio na Global TV Online kilichofanyika kwenye Hoteli ya The Atriums iliyopo Sinza Africasana jijini Dar.

 

Alisema, kabla ya kuwa maarufu, wapo baadhi ya watu ambao hawakuwa na utu walimtenga na kumnyanyasa kutokana na uelewa wao.


“Ni kutokana na kukosa elimu, ndio maana nasisitiza bado tunao wajibu wa kuwaelimisha. Kwenye tamthiliya ya Jua Kali inayorushwa DStv, nimecheza karibu asilimia 60 hadi 70 ya maisha yangu ili kutoa elimu na jamii kuacha kuwanyanyasa watu wenye maumbile kama yangu,” alisema Dorah.

 

Mbali na hilo, Dorah alizungumzia pia kuhusu maisha yake ya mahusiano ambapo alisema kwa sasa hana mtu lakini, mama yake mlezi na dairekta wake, Lamata (Leah Mwendamseke) anamuongoza vyema katika kumpa nasaha zinazomjenga na muda ukifika akapata mchumba basi bila shaka atafuata taratibu stahiki.

 

Dorah pamoja na Lamata wamezungumza mengi katika mahojiano hayo, kuyapata kwa kina, ingia Global TV Online ili upate uhondo kamili.

STORI: ERIC EVARIST |GPL

Leave A Reply