The House of Favourite Newspapers

Drake Anunua Mjengo Bil.197

0

USISEME hatuna pesa, bali sema sina pesa! Taarifa ikufikie kwamba, rapa wa kiwango cha dunia, Drake anayepiga mbishe zake pale kwa Rais Joe Biden wa Marekani ndiye anayetengeneza vichwa vya habari kwa sasa baada ya kununua mjengo wa kifahari wenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 85 ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 197 za Kitanzania.

 

Kwa mujibu wa mitandao ya burudani ya kimataifa, mjengo huo upo pande za Beverly Hills mjini Los Angeles, Marekani na una jumla ya ukubwa wa square feet 25,000.

Pia unaelezwa kwamba una vyumba 10 vya kulala,, bafu 22, garage za magari 11, gym na uwanja wa mchezo wa tenisi na vikorokoro vingine vingi.

Stori: Sifael Paul

 

Leave A Reply