The House of Favourite Newspapers

Drogba Kutundika Daruga Mapema Ili Kuinusuru Chelsea?

0

DrogbaDidier Drogba akiwa na Guus Hiddink Kwenye Uwanja wa Stamford Bridge

Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea na timu ya taifa ya Ivory Coast, Didier Drogba anaangalia uwezekano wa kutundika daruga haraka ili kuitikia wito wa kujiunga na benchi la ufundi linaloongozwa na kocha Mholanzi Guus Hiddink, Stamford Bridge.

Drogba-1Didier Drogba akishangilia ushindi kwenye moja ya mechi za Premier League.

Kocha Guus Hiddink amempa nafasi mchezaji huyo wa zamani wa klabu hiyo kujiunga nae na kuwa sehemu ya benchi la ufundi la timu hiyo ili kuongeza mahusiano mazuri kati ya wachezaji na benchi hilo.

Lakini taarifa zilizochapishwa nchini Ufaransa hivi karibuni kuwa tayari Didier Drogba amestaafu soka, zimekanushwa na kwamba mshambuliaji huyo wa Montreal ndio kwanza anafikiria uwezekano wa kufanya hivyo.

Didier Drogba alipata kuichezea Chelsea kwa misimu kadhaa huku akiweka rekodi ya kuwa mchezaji pekee kutoka Afrika kufunga magoli 100 katika historia ya ligi kuu nchini England, huku akiisaidia klabu ya Chelsea kushinda mataji mengi ikiwemo lile la ubingwa wa vilabu barani Ulaya.

Leave A Reply