The House of Favourite Newspapers

DROO KUBWA YA SHINDA NYUMBA…MWISHO WA UBISHI LEO LAS VEGAS MABIBO

0

DROO kubwa ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili, itachezeshwa leo Jumatano katika Viwanja vya Las Vegas vilivyopo Mabibo mkabala na Soko la Ndizi jijini Dar es Salaam. Meneja Mkuu wa Kampuni ya Global Publishers, Abdallah Mrisho ambayo ndiyo inaendesha zoezi hilo, alisema jana kuwa hafla hiyo itachagizwa na burudani kutoka kwa madensa maalum walioandaliwa kabla ya wakati wa kumsaka mshindi wa mjengo wenye thamani ya mamilioni uliojengwa Bunju B haujawadia.

Nyumba hiyo ni ya kisasa yenye vyumba vitatu vya kulala, kikiwemo kimoja ambacho ni Master Bed Room. Licha ya vyumba hivyo vitatu, ndani ya mjengo huo pia kuna sebule, chumba cha maakuli, jiko na vyoo ndani, kitu ambacho kitamfanya mmiliki wake akiingia ameingia.

Lakini kitu cha kufurahisha zaidi kuhusu nyumba hii ni kwamba mmiliki wake, ambaye atakuwa ni yule atakayeibuka mshindi katika droo kubwa ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili, hatakuwa na haja ya kuhangaika kuweka umeme, kwani atakuta umeingizwa tayari kwa matumizi.

“Lengo letu siku zote ni “Tumekamilisha kila kitu, kilichobakia sasa ni kuwaomba wasomaji wa magazeti yetu ya Ijumaa Wikienda, Amani, Uwazi, Risasi, Championi na Ijumaa kujitokeza kwa wingi leo katika viwanja hivyo kuweza kumshuhudia mshindi, bila kusahau pia kutakuwepo na zawadi ndogondogo za sapraiz,” alisema Meneja Mrisho. Nyumba hiyo ya kisasa imejengwa Bunju B, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam ikiwa na thamani ya mamilioni ya shilingi na itakuwa ni ya pili kutolewa na Global Publishers, kwani katika bahati nasibu ya kwanza iliyofanyika mwaka jana, kurejesha faida kidogo tunayopata kwa jamii tunayofanya nayo kazi, ndiyo maana tumeingia gharama kubwa kuijenga nyumba hii iwe ya kisasa, ili mtu atakayebahatika kuipata, abadili kweli maisha yake na hiyo ndiyo kauli mbiu yetu, kubadili maisha ya watu.

“Ni nyumba ya kisasa kwa vigezo vyote, vyumba vitatu vya kulala, sebule kubwa, chumba cha chakula, jiko, choo, bafu vyote hivyo vitapatikana ndani ya nyumba, mmiliki wake atakabidhiwa hati ya kiwanja na ataukuta umeme umeingia, kazi yake itakuwa ni kuweka luku ili aendelee na huduma hiyo.


mjengo wa aina hiyo ulitolewa. Aliyeshinda katika bahati nasibu hiyo ya kwanza alikuwa ni mwanamama mjasiriamali, Nelly Mwangosi mwenyeji wa Iringa ambaye mjengo wake ulijengwa eneo la Salasala, pia nje ya jiji. Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili inafanyika baada ya kuwepo kwa droo ndogo tano zilizochezeshwa katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam ambako zaidi ya wasomaji 30 wa magazeti ya Championi, Ijumaa, Risasi, Uwazi, Amani na Ijumaa Wikienda waliibuka na zawadi za aina mbalimbali zikiwemo pikipiki, televisheni kubwa, simu za kisasa za mikononi, dinner set na ving’amuzi.

Leave A Reply