The House of Favourite Newspapers

Droo ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika kuchezwa leo

0

Droo ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) na kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC) inatarajiwa kuchezwa leo Oktoba 6, 2023 majira ya saa 9:00 alasiri mjini Johannesburg, Afrika Kusini huku vigogo 16 waliofuzu hatua hiyo wakitarajiwa kubaini wapinzani wao kwenye hatua ya makundi.

Mbivu na mbichi kujulikana leo huku shauku kubwa ya mashabiki wa soka Tanzania ni kubaini kama wawakilishi wa Tanzania kwenye CAFCL, Simba SC na Yanga SC watapangwa kwenye kundi moja.

Watani hao wa jadi wamepangwa kwenye vyungu tofauti kuelekea upangaji huo wa makundi huku Simba SC ikipangwa kwenye chungu (Pot) namba 2 sambamba na CR Belouizdad ya Algeria, Pyramids ya Misri na Petro Atletico ya Angola.

Kwa upande wake Young Africans SC wamepangwa kwenye chungu namba 3 sambamba na TP Mazembe ya DRC, Al Hilal SC ya Sudan na Asec Mimosas ya Ivory Coast.

Kikanuni upo uwezekano wa Simba SC na Yanga SC kupangwa kundi moja kwasababu ‘kila kundi litaundwa na timu moja kutoka kila chungu kati ya vinne.’

Kanuni ya CAF kuhusu upangaji makundi inasema “Chama cha mpira hakiwezi kuwa na timu zaidi ya mbili kutoka nchini mwake kwenye hatua ya makundi”. Hivyo hakuna kizuizi cha timu mbili kutoka Taifa moja kukutana kwenye kundi moja.

VYUNGU (POTS) KUELEKEA DROO YA MAKUNDI CAFCL

POT 1.
🇪🇬 Al Ahly
🇲🇦 Wydad
🇹🇳 Esperance
🇿🇦 Mamelodi

POT 2.
🇩🇿 Belouizdad
🇪🇬 Pyramids
🇦🇴 Petro Atletico
🇹🇿 Simba SC

POT 3.
🇹🇿Yanga SC 🇹🇿
🇨🇩 TP Mazembe
🇸🇩 Al Hilal SC
🇨🇮 ASEC

POT 4.
🇹🇳 Etoile Sahel
🇧🇼 Jwaneng Galaxy
🇲🇷 FC Nouadhibou
🇬🇭 Medeam

Leave A Reply