The House of Favourite Newspapers

Duh! Kwa Zawadi Hizi… GLOBAL APP Wametisha Mbaya – Video

APPLICATION namba moja kwa habari Tanzania, GLOBAL APP imeendelea kuwajali wasomaji wake kupitia shindano lake mahsusi la PAKUA USHINDE, baada kuwamwagia zawadi washindi shindano hilo akiwano Amos Anthony, mkazi wa Tabata jijini Dar es Salaam aliyejishindia tablet mpya pamoja na washindi wengine watano wa muda wa maongezi.

 

Akizungumza katika studio za Global TV Online zilizopo Sinza-Mori jijini Dar es Salaam mara baada ya kupokea zawadi yake, mshindi wa tablet, Amos alisema:

“Wakati ninaanza kushiriki shindano la Pakua Ushinde sikuwa ninaamini kama kweli nitashinda, lakini imani iliniijia siku niliyopigiwa simu kwamba nimeshinda.  Kwa kweli nilifurahi sana, na mpaka leo ninapopokea zawadi hii ninajiona mwenye bahati na furaha kubwa.

Amos Anthony (kushoto) baada ya kukabidhiwa zawadi yake akiwa na Mratibu wa PAKUA USHINDE, Joseph Makuka.

“Ndani ya Global App ninapenda zaidi magazeti hasa ya michezo, taarifa zilizomo ndani ya Global App ni nzuri na ni za uhakika na ukweli. Kwa watu ambao hawajaanza kutumia Global App au kupakua, ninawashauri wafanye hivyo sasa kwani wanapitwa na vitu vingi vizuri. Pia, wanaweza kushinda kama mimi na kupata zawadi ambazo zitakuwa na manufaa makubwa kwao.”

 

Mbali na Amos, wengine walioibuka washindi kwenye PAKUA USHINDE ni Arzaki Mlipu (Kongwa Dodoma), Matilda Mwasha (Moshi), Bertwiner Musiba (Ilemela Mwanza), Doris Tungaraza (Singida) na Abuu Mnebe (Morogoro) ambao wote hawa walijishindia muda wa maongezi wa shilingi 10,000 kila mmoja.

 

Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hiyo, Mratibu wa PAKUA USHINDE, Joseph Makuka alisema GLOBAL AAP ambayo inakimbiza kwa sasa Bongo, imerahisisha upataji na usomaji wa habari za kila siku kuhusu mastaa, burudani, matukio ya kijamii, siasa habari za magazeti ya Tanzania za kila siku.

“Global App imekurahisishia upataji wa BREAKING NEWS mara tu zinapotokea kwa kupokea Notification kwenye simu yako ya kiganjani. Ndani ya App hii kuna Global TV ikikuletea video zote kali za kila siku, Matukio LIVE ya mikutano ya Rais Dkt. John Magufuli, viongozi mbalimbali, mastaa wa Bongo, na matukio yote makubwa,” alisema Makuka.

 

Aidha, utaweza kusoma hadithi za Eric Shigongo kwa mfumo wa maandishi na kusikiliza hadithi hizo kwa mfumo wa audio. Pia kuna video zote mpya za muziki wa Bongo Fleva na Mamtoni, michezo na makala za mapenzi, maisha na afya unazipata ndani ya GLOBAL APP ambayo ipo kwenye Play Store na App Store.

Install GlobalApp

Android: ==>  bit.ly/2AAQe1d

iOS: ===> apple.co/2Assf4M

TAZAMA MSHINDI AKIKABIDHIWA TABLET YAKE MPYAAA!

Comments are closed.