The House of Favourite Newspapers

Dulla Makabila: Manara ulinirubuni, Nirudishe Ulikonitoa

0

MSANII wa Singeli nchini Dulla Makabila, amemlalamikia Msemaji wa Yanga Haji Manara kwa kitendo chake cha kumshawishi mpaka kumhamisha kutoka kuishabikia Yanga Sc na kuhamia kuishabikia Simba Sc na baadaye Manara akatimka Simba na kuhamia Yanga huku akimtelekeza Makabila.

 

Dulla Makabila alikuwa ni Shabiki wa Yanga lakini kutokana na ushawishi wa Haji ambae alikuwa ni Msemaji wa Simba wakati huo akajikuta anahamia Simba na wimbo wa kuisifia Simba akautoa.

 

Sasa leo Februari 5, Dulla Makabila amemlalamikia haji akidai kwamba alimrubuni kuhamia katika klabu hiyo. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Dulla ameandika ujumbe kwenda kwa Haji na Wanayanga akiomba kurudi Yanga ili afurahie maisha ya soka kama zamani.

Leave A Reply