The House of Favourite Newspapers

Esha Buheti Atamani Kumpamba Rais Samia

0

MWANAMAMA mwigizaji wa Bongo Movies na mjasiriamali, Esha Buheti anasema amehitimu mafunzo ya utengenezaji wa keki zitakazokuwa gumzo kwa kuwa atazitengeneza kwa staili ya sura ya mhusika.


Akizungumza na IJUMAA,
Esha amesema kuwa, baada ya mafunzo hayo, sasa anatamani kutengeneza keki itakayokuwa na nakshi zilizopambwa na picha ya Rais Samia Suluhu Hassan.


Esha anasema kuwa, moja ya
ujuzi aliopata katika mafunzo hayo ni upikaji keki kwa kutengeneza picha na maumbo ya vitu mbalimbali.


Anasema ili kupima ujuzi
wake, atatengeneza keki maalum atakayoipamba kwa picha ya sura ya Rais Samia na kama itawezekana atampatia kama zawadi.


“Nimepata mafunzo ambayo
yameongezea kipaji changu cha kupika, napenda sana kupika ndiyo maana napambana ili niwe mpishi bora mwenye vyakula vilivyoandaliwa kwa ustadi mkubwa,” anasema Esha.


Anaongeza kuwa, licha ya kuwa
na ndoto ya kumtengenezea keki Rais, anatamani pia kumnadi mwanamuziki Nasibu Abdul au Diamond Platnumz kwa kuuza keki zenye picha ya sura yake.


Esha amewataka vijana
kuchangamkia fursa zinazopatikana au mafunzo yanayotolewa na wakufunzi wa masuala mbalimbali kwa ajili ya kuongeza ujuzi.


Msanii huyo alikuwa miongoni
mwa watu 15 waliopata mafunzo ya siku tano ya upishi wa keki jijini Dar yaliyotolewa na mpishi maarufu aitwaye Tuba Geckil kutoka Uturuki.

STORI; ELVAN STAMBULI, DAR

Leave A Reply