The House of Favourite Newspapers

Ebola Yaripotiwa Kuingia Guinea

0

Guinea imeripoti maambukizi ya ugonjwa wa #Ebola ambapo watu wanne wameripotiwa kufariki dunia hadi sasa. Idara ya Afya ya Taifa imesema watu hao walianza kuugua, kutapika na kuvuja damu baada ya kuhudhuria mazishi katika Wilaya ya Goueke.

 

 

Vipimo vinaendelea ili kuthibitisha maambukizi na wahudumu wa Afya tayari wanawafuatilia wote waliokutana na wagonjwa hao. Ebola iliua zaidi ya watu 11,000 kati ya 2013 hadi 2016 ambapo baadae ilidhibitiwa.

Leave A Reply