The House of Favourite Newspapers

Ed Sheeran Atangaza Kupumzika Muziki

Image result for ed sheeran

MWANAMUZIKI maarufu duniani, Mwingereza, Edward Christopher Sheeran,  maarufu kama  Ed Sheeran ametangaza kuwa atapumzika kazi hiyo baada ya kuifanya kwa muda mrefu.

Ametoa kauli hiyo  alipokuwa anafanya hitimisho la ziara yake ya ‘Divide World Tour’ mjini Ipswich, Uingereza, baada ya miaka miwili ya kuzunguka na ziara yake hiyo yenye mafanikio zaidi kwa muda wote .

“Nimependa uwepo wenu hapa na tumemaliza ziara yetu mjini Ipswich. Hili ni tamasha langu la mwisho kwa takribani miezi 18,” alisema.

Hii ni baada ya watu zaidi ya milioni tisa kuhudhuria kwenye tamasha lake la ‘Divide World Tour’ lililoanza mwezi Machi mwaka 2017 ambapo ndani ya siku 893 amezunguka mataifa 46 kwenye miji 175 na kufanya shoo 260,  akiwa na crew ya watu 268 na kutembea kilometa 311,029 zilizomwingizia kiasi cha Sh. trilioni 1.9 za Tanzania.

Comments are closed.