The House of Favourite Newspapers

MAHARI YA POSHY BEI CHEE!

MREMBO mwenye umbo matata Bongo, Jacqueline Obeid ‘Poshy Queen’ amesema pindi utakapofika wakati wa kuolewa, hataki mahari kubwa ili baadaye isije kutumika kama fimbo ya kumchapia.

Akizungumza na Amani, Poshy alisema watu wengi wanafikiri msichana ukitolewa mahari kubwa ni sifa kumbe ni kujitengenezea wakati mgumu mbele ya safari kwa mwanaume kukutumikisha akiamini amekununua kama bidhaa.

“Kama nina mtu wangu nampenda na yeye ananipenda kwa nini tusikubaliane tu wazazi wakatutambua, na ikifika hatua ya kufunga ndoa mahari yangu nataka bei ya kawaida tu maana wengine hata elfu thelathini anaolewa na anaishi vizuri lakini sio kila kukicha mtu anakufanyia vitendo vibaya ndani ukimuuliza anakuambia kakutolea mahari kubwa, mimi hiyo sitaki hata elfu hamsini naolewa tu,” alisema Poshy.

Comments are closed.