The House of Favourite Newspapers

EFF yatua kuwakomboa wachezaji Bongo

0

Hans Mloli,
Dar es Salaam
INAWEZA kuwa habari njema kwa wachezaji na wadau wa soka la Bongo baada ya taasisi inayojulikana kwa jina la Enlightened Football Foundation (EFF) kuweka wazi jinsi wanavyoweza kuwasaidia wachezaji, makocha na hata mameneja jinsi ya kurahisisha mambo na kupata mafanikio kupitia mchezo huo.

Kwa miaka ya hivi karibuni ingawa soka limeonekana kukua kwa maana ya ushabiki lakini wahusika wanaonekana kunyonywa na kushindwa kuhimili maisha, taasisi hiyo imekuja na mifumo mbadala ambayo imedokeza michache kati ya mingi waliyonayo katika kuhakikisha wanatumia nafasi waliyonayo kuliinua soka la Bongo.
Mtendaji Mkuu wa EFF, Daniel Mwakasungula ameliambia gazeti hili kuwa taasisi hiyo ambayo ilisajiliwa rasmi Novemba 11, 2015, inajishughulisha katika kurekebisha vipengele vya mikataba, kuwatengeneza vijana wachanga kukua katika
msingi ya soka, namna ya kukusanya pesa nje ya mshahara wao kupitia vipaji vyao na mengine mengi.
“Ofisi zetu zipo pale Kinondoni Kwa Manyanya na kwa kifupi tupo kwa ajili ya kuendeleza soka nje ya uwanja kwa kutoa elimu, kuelekeza baadhi ya mambo ambayo ni vikwazo kwa wachezaji, makocha au mameneja, haya yote yanafanyika bure.
“Tuna mawakili pale ambao watawaelimisha na kupitia mikataba ya wachezaji au makocha kabla ya kutia saini, lakini kumjuza na kumwelewesha kijana juu ya kazi yake, nini afanye, ajitunze vipi ili afikie malengo na pia kuwa na umuhimu wa mameneja wanaofahamu kazi zao na mengine mengi,” alisema Mwakasungula.

Leave A Reply