The House of Favourite Newspapers

Efm Yacheza Mechi na Madereva Daladala Kiwanja cha Tanganyika Packers

0

Kituo cha utangazaji cha EFM redio  kimecheza mechi ya kirafiki baina yao na madereva daladala siku ya leo ya tarehe 24/05/2017 katika Kiwanja cha Tanganyika Packers kuanzia saa kumi Jioni, ambapo watangazaji  wa Redio hiyo wamechuana vilivyo na wadau wao wakubwa.

Redio hii ya vijana na jamii kwa ujumla imezidi kutoa kipaumbele kwenye michezo hususani mpira wa miguu kwani imekua ikicheza mechi nyingi za kirafiki kila inapobidi ili kuhakikisha inajenga mahusiano mazuri na jamii inayoizunguka kama wadau wa taasisi mbalimbali ili kukuza vipaji vyao.

Mechi hizi za kirafiki ni kati ya michezo ambayo husaidia jamii kukutana kwa pamoja na kujenga mahusiano mazuri na vile vile husaidia kuhamasisha vijana kufanya mazoezi katika kuunga mkono kampeni ya serikali ya kufanya mazoezi  katika jamii ili kujiepusha na hatari ya kupata magonjwa yasioambukizwa.

 

Leave A Reply