The House of Favourite Newspapers

Elewa Kinachosababisha Kuwa na Kizunguzungu (Dizziness)

0

Kizunguzungu kisichofahamika chanzo (Benign Paroxysmal Positional Vertigo) – Kizunguzungu hiki hakina athari kubwa kwa maisha ya muhusika. Aina hii ya kizunguzungu hakifahamiki chanzo chake (idiopathic), kwa lugha nyepesi tungesema cha kuzaliwa nacho. Hutokea pale mtu anapobadili mkao ghafla; kuamka na kukaa kitandani ghafla au kusimama ghafla kwa mtu aliyekuwa ameketi. Pia kugeuza au kuinamisha au kuangalia juu haraka.

Uambukizo; Mishipa ya fahamu ya sehemu ya ndani ya sikio inapopata uambukizo wa aina fulani ya virusi na kusababisha kizunguzungu na wakati mwingine hata kutosikia sawa sawa.

Kujaa kwa majimaji sehemu ya ndani ya sikio (Meniere’s disease); hapa tunamaanisha maji yanayotengenezwa ndani ya sikio kwasababu fulani fulani huzidi kiwango kinachokubalika na kusababisha kizunguzungu ambacho hudumu kwa masaa kadhaa. Pia huleta kuziba na kuzibuka kwa masikio, sauti za kengele na kuhisi kama vile sikio limezibwa kwa pamba.

Kipanda uso (Migraine). Watu wanaopata matatizo ya kipanda uso hupata pia kizunguzungu hata kama kwa wakati huo kichwa hakiumi. Kizunguzungu wanachopata hawa huwa kina dumu kwa dakika hadi saa kadhaa na kupotea. Pia wanakuwa na hali ya kutotaka makelele, sauti ndogo wao huhisi ni kelele kubwa sana.

MATATIZO YA MZUNGUKO WA DAMU UNAVYOWEZA KULETA KIZUNGU

ZUNGU

Kushuka kwa shinikizo la damu (Low Pressure). Kushuka kwa ghafla kwa shinikizo la damu kunaleta kizunguzungu cha muda mfupi. Hali hii inaweza kutokea iwapo utasimama ghafla kama ulikuwa umeketi au kuamka na kuketi kitandani ghafla. Kubadilika kwa mkao wa mwili huku kunasababisha shinikizo la damu lishuke ghafla kwani mwili unakuwa haujapata muda wa kujiweka sawa.

Matatizo ya kutozunguuka vyema kwa damu; huku kunatokea kwa watu wenye magonjwa ya moyo kuwa mkubwa (Cardiomyopathy), shambulio la moyo (Heart attack), na mapigo ya moyo yaliyoparaganyika (Arrhythmia). Matatizo haya yote yanababisha moyo ambao ndiyo pump, kupungua uwezo wa kusukuma damu ya kutosha kwa ajili ya mahitaji ya mwili, ikiwemo ubongo na sehemu ya ndani ya sikio.

SABABU ZINGINE ZINAZOLETA KIZUNGUZUNGU

Magonjwa ya mishipa ya fahamu Dawa zinazotumika kutibia matatizo mbalimbali yanaweza kuwa chanzo cha kizunguzungu. Mfano dawa za kuzuia degedege, dawa za sonona, na dawa za kutibu shinikizo la damu pia huwa ni sababu kwani kuna wakati hushusha shinikizo la damu kufikia chini ya kiwango.

Aina fulani ya magonjwa yanayomfanya mtu kuwa na wasiwasi kuliko kawaida huleta kizungunguzu.Upungufu wa damu. Kupungua kwa wekundu wa chembechembe nyekundu za damu huleta kizungunguzu kwani kiwango cha hewa ya oxygen kinachozunguuka kinakuwa kidogo.

Kushuka kwa sukari. Hali hii huwapata watu wenye kisukari wanaotumia insulin ambayo inaweza kusababisha sukari kushuka sana. Pia hata wenye njaa kupita kiasi.

Joto kali na kupungukiwa maji. Joto kali husababisha kutokwa na jasho jingi hivyo maji mwilini kupungua na kuleta kizunguzungu.

ATHALI

Athari kubwa za kizunguzungu zinakuja pale ambapo kizunguzungu kinapoweza kusababisha muhusika kuanguka chini. Kitendo cha kuanguka kinaweza kuleta majeraha mbalimbali mwili kulingana na namna na mahala alipoangukia muhusika. Athari nyingine ni za kiuchumi na kijamii pale ambapo kizunguzungu kikiwa cha muda mrefu na kusababisha muhusika ashindwe kushiriki shughuli za kumuingizia kipato na za kijamii.

UTAMBUZI

Utambuzi wa matatizo yanayoleta kizunguzungu yatahusisha uchukuaji wa maelezo na kufanya vipimo ambavyo daktari ataona vinafaa.

MATIBABU

Yatategemeana na chanzo kilichogundulika. Matibabu yanaweza kuhusisha dawa, upasuaji na mazoezi.

 

 

Leave A Reply