The House of Favourite Newspapers

Elias Maguli apata dili Ufaransa

0

Elius-Maguli1
Sweetbert Lukonge,
Dar es Salaam
SIKU yoyote kuanzia sasa, mshambuliaji wa Stand United ya Shinyanga, Elias Maguli anaweza kutimkia zake nchini Ufaransa kwa ajili ya kwenda kutafuta nafasi ya kucheza soka la kulipwa.

Maguli ambaye anaongoza kwa mabao katika Ligi Kuu Bara akiwa na mabao nane, amepata dili la kwenda kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa katika moja ya timu za daraja la pili nchini humo.
Inadaiwa kuwa, timu hiyo imefikia hatua hiyo ya kumuita Maguli baada ya kuvutiwa na uwezo wake anaouonyesha siku za hivi karibuni.
“Tunamshukuru Mungu kuwa timu yetu ya Stand hivi sasa nayo inatambulika kimataifa, nasema hivyo kwa sababu tumepokea ofa kutoka timu moja ya Ufaransa ambayo inamhitaji Maguli kwa ajili ya majaribio,” kilisema chanzo.
Alipotafutwa Maguli alisema: “Kweli nimepata dili la kwenda kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa nje ya nchi lakini siwezi kusema ni wapi huko kwa sababu mambo bado hayajakaa sawa.”

Leave A Reply