The House of Favourite Newspapers

Simba wabeba pointi za Majimaji mapema

0

SIMBA (7)
Mohammed Mdose,
Dar es Salaam
JAPOKUWA mechi bado haijachezwa, lakini unaweza kusema kuwa tayari Simba wameshajibebea pointi tatu kutoka kwa wapinzani wao timu ya Majimaji kwenye mchezo wao wa kesho Jumamosi.

Simba ambayo inanolewa na Dylan Kerr wa Uingereza na Majimaji inayonolewa na Mika Lonnstrom raia wa Finland zinatarajiwa kukutana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar katika Ligi Kuu Bara.
Bosi wa Majimaji, Lonnstrom ameweka wazi kuwa wanakuja Dar kupambana huku wakijua hawana uwezo wa kuizuia Simba isishinde kwenye mchezo huo.
“Tunaenda kucheza na Simba ambayo kiukweli ni timu kubwa, hivyo itakuwa ni ngumu sana kuizuia isiibuke na ushindi katika mchezo huo, lakini siyo kwamba tutaingia kinyonge bali tutapambana mwanzo-mwisho tuone kitakachotokea,” alisema Lonnstrom.

Leave A Reply