The House of Favourite Newspapers

ENGLAND KUIVAA CROATIA NUSU FAINALI

CROATIA itaivaa England kwenye nusu fainali ya Kombe la Dunia baada ya kuwatoa wenyeji Urusi kwa penalti 4-3 kwenye mechi ya robo fainali iliyofanyika kwenye Uwanja wa Fisht mjini Sochi jana Jumamosi.

 

Baada ya mchezo huo kumalizika kwa sare ya mabao 2-2 kwenye dakika 120 za mwanzo, Croatia inayotinga kwa mara ya pili kwenye nusu fainali ya Kombe la Dunia, ilipoteza penalti moja kutokana na kipa wa Urusi, Igor Akinfeev kuokoa mkwaju wa Mateo Kovacic.

Wenyeji wa Urusi walipoteza penalti mbili baada ya ile ya Fedor Smolov kuokolewa na kipa wa Croatia, Danijel Subasic na Mario Fernandez kupiga nje. Croatia itaivaa England iliyoitoa Sweden baada ya kuifunga mabao 2-0 mapema jana kwenye mechi itakayopigwa Jumatano ijayo kwenye Uwanja wa Luzhniki mjini Moscow.

Ufaransa na Ubelgiji zitavaana kwenye mchezo mwingine wa nusu fainali utakaopigwa keshokutwa Jumanne mjini St. Petersburg. Urusi ndio ilitangulia kufunga bao mnamo dakika ya 31 lililofungwa na Denis Cherychev kufuatia pasi ya Artem Dzyuba.

 

Croatia baada ya ile ya Fedor Smolov kuokolewa na kipa wa Croatia, Danijel Subasic
ilisawazisha katika dakika ya 39 kwa bao lililofungwa kwa kichwa na Andrej Kramaric baada ya kuunganisha krosi maridadi ya Mario Mandzukic.

Baada ya timu hizo kufungana bao 1-1 kwenye muda wa 90 za kawaida, Croatia ilipata bao la pili katika dakika ya 101 baada ya Luka Modric kupiga mpira wa kona uliounganishwa wavuni kwa kichwa na Domagoj Vida.

 

Urusi ilisawazisha baada ya Alan Dzagoev kupiga mpira wa faulo uliounganishwa wavuni kwa kichwa na Fernandes mnamo dakika ya 115

Comments are closed.