The House of Favourite Newspapers

Ennovate Yatoa Ofa Ya Ufadhili Kwa Mwenye Wazo La Mradi

0
Mkurugenzi wa Miradi wa Ennovate Hub, Faraji Emily akizungumza na wanahabari (hawapo pichani).

Kampuni ya Ennovate Hub ya Jijini Dar es Salaam leo imezindua mpango wake wa kuwasaidia wajasiriamali wenye mawazo ya kuanzisha miradi mbalimbali lakini kushindwa kufikia malengo yao kutokana na changamoto.

Akizungumza kwenye mkutano na wanahabari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Miradi wa Kampuni hiyo, Faraji Emily amesema uzinduzi wa mpango huo una lengo la kuwasaidia wajasiriamali wanaoshindwa kufikia malengo yao kutokana na changamoto mbalimbali.

Afisa Miradi wa kampuni hiyo Moureen Mollel akiwasisitiza vijana wa hapa nchini na nje ya nchi wanaosaka ajira kuchangamkia fulsa hiyo. 

Faraji alizitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na kukosa mitaji, wataalamu wa kuyaboresha mawazo yao na mambo mengine.

Mkurugenzi huyo amesema kupitia mpango huo watawapatia wajasiriamali hao wafadhili, mitaji, wataalamu na mambo mengine yanayohitajika na kusema fulsa hiyo ni kwaajili ya wasiriamali wa hapa nchini, Afrika Mashariki na hata nje ya Bara la Afrika. Baada ya kusema hayo amewataka wenye mawazo ya miradi haswa vijana ambao ndiyo nguvu kazi ya sasa kuchangamkia fulsa hiyo kwa kuingia kwenye website yao kupata maelekezo zaidi ambayo ni www.ennovatehub.com

Mkutano huo ukiendelea.

Akisisitiza hilo Afisa miradi wa kampuni hiyo, Moureen Mollel naye amewasisitiza vijana wa kitanzania ambao ndiyo nguvu mpya kuchangamkia fulsa hiyo ili waweze kutimiza ndoto zao.

Sehemu ya bango la kampuni hiyo.

Mollel amesema fulsa hiyo itawakomboa wajasiriamali wengi wenye mawazo ya miradi.

HABARI/PICHA:RICHARD BUKOS /GPL

Leave A Reply