The House of Favourite Newspapers

Erycah aifungukia siku yake ya kwanza faragha

0

erycahWIKI hii kwenye safu yetu ya 10 Questions tunaye video queen anayekuja kwa kasi Bongo, huyu si mwingine bali ni mwanadada anayefahamika kwa jina la Ericka Daniel Moshi ‘Erycah. Anafunguka mambo mbalimbali kupitia maswali aliyoulizwa na Mwandishi Wetu Gabriel Ng’osha. Fuatilia hapa chini…

Ijumaa: Habari ya mjini ni kwamba uli-date na msanii Linex baada ya kumaliza kufanya naye ile video ya Kwa Hela, una lipi la kujitetea?

Erycah: Si kweli na napenda Watanzania wajue kuwa sijawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Linex zaidi ya ule wa kikazi tu.

Ijumaa: Hivi ni kwa nini uliamua kujiingiza kwenye kazi ya ‘kuuza nyago’ na si kazi nyingine?

Erycah: Niligundua kuwa, kwa muonekano wangu ningeweza kufanya vizuri ndiyo maana nikaamua kuja huku..

Ijumaa: Kama si u-video queen unadhani ungekuwa unafanya shughuli gani kwa sasa?

Erycah: Kwa kuwa napenda sana biashara basi ningejikita kwenye ujasiriamali.

Ijumaa: Hadi kufikia hapo ulipo umeshawahi kutoka na wanaume wangapi?

Erycah: Kusema ule ukweli kabisa ni watatu tu. Nione hivihivi lakini ni msichana ninayeuthamini sana mwili wangu.

Ijumaa: Ni yupi ambaye umewahi kumpenda kati ya wote na kwamba uliumia sana mlipoachana?

Erycah: Naomba nisimtaje maana at ajisikia sana huko aliko na najua tayari ana mtu mwingine.

Ijumaa: Mara ya kwanza kabisa kukutana faragha na mpenzi wako ilikuwaje?

Erycah: Sijui hata nisemeje kwa kuwa nilipata wakati mgumu ambao hauelezeki. Sitaki hata kukumbuka siku yangu ya kwanza faragha.

Ijumaa: Kwani uliingia kwenye uhusiano wa kwanza wa kimapenzi ukiwa na umri wa miaka mingapi?

Erycah: Dah! Maswali mengine bhana! Nilikuwa na miaka 18.

Ijumaa: Nini kinakuumiza kwenye mapenzi?

Erycah: Kudanganywa kama mtoto mdogo sipendi kabisa.

Ijumaa: Wengi wanaoonekana wakiuza nyago kwenye video za wasanii wameishia la saba na wengine kidato cha nne, wewe elimu yako ikoje?

Ericka: Nimemaliza diploma ya Record Management pale Chuo cha Magogoni, kama Mungu akijalia mwakani nitaendelea.

Ijumaa: Mavideo queen wengi wanadaiwa kuitumia fani hiyo kujiuza, kwako hilo likoje?

Erycah: Unajua kila mmoja ana akili zake, mimi nafanya kazi hii kama zilivyo nyingine sasa kama wapo wanaojiuza kwa staili hiyo ni wao na maisha yao.

Leave A Reply