The House of Favourite Newspapers

Esma: Akiolewa Wema Itakuwa Poa

MWANADA-SHOSTI ambaye ni dada wa staa wa Afro-Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ Esma Khan ‘Esma Platnumz’ amefunguka kuwa, kama kaka yake ataamua kurusha karata yake kwa mkali wa Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu na kufunga naye ndoa itakuwa poa tu.

Akipiga stori na Over Ze Weekend, Esma alitoa la moyoni kuwa kwa upande wake, hawezi kumchagulia kaka yake mke, lakini kama ataamua kurudisha majeshi kwa mpenzi wake wa zamani, Wema atafurahi zaidi.

 

“Unajua Nasibu (Diamond) ndiye anajua zaidi mke anayemfaa, lakini kama pia ataamua kurudi kwa Wema, mimi nitafurahi tu kwa sababu ni mtu ambaye tunapatana sana na ninampenda pia,” alisema Esma.

 

Kumekuwa na sintofahamu ya nani atakayeolewa na Diamond baada ya kutengana na mzazi mwenzake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ na kutangaza kuwa atafunga ndoa mwezi Juni, mwaka huu.

 

IMELDA MTEMA.

Comments are closed.