The House of Favourite Newspapers

Esma: Natamani Mama Dangote Angezaa Mtoto Mwingine

0
Mwanamama maarufu kwenye mitandao ya kijamii na dada wa staa wa muziki wa Kizazi Kipya nchini Tanzania, Diamond Platnumz, Esma Platnumz.

 

Esma Platnumz; ni mwanamama maarufu kwenye mitandao ya kijamii na dada wa staa wa muziki wa Kizazi Kipya nchini Tanzania, Diamond Platnumz ambaye ameibuka na jipya.

 

Esma na Diamond wamezaliwa wawili tu kwa mama yao, Mama Dangote japokuwa baba ni tofauti.

Esma baba yake anaitwa Khan ambaye ni mtu wa Zanzibar mwenye asili ya Kiarabu huku Diamond baba yake aliitwa Salum Nyange.

Esma anasema kuwa, anatamani sana mama yake, Mama Dangote angezaa mtoto mwingine maana walitoka wawili tu kwenye tumbo la mama yao; yeye pamoja na Nasibu (Diamond).

 

Mama huyo wa watoto wawili anasema kuwa, atafurahi mno mdogo wake huyo atakayezaliwa awe ni wa kike.

Mama Dangote ambaye ni mke halali wa ndoa wa Shamte ameshavuka umri wa kuweza kupata mtoto kwa sababu ana umri wa zaidi ya miaka 50 kwa sasa.

STORI NA SIFAEL PAUL | GPL

MAKOCHA SIMBA, AZAM WAZUNGUMZA NA WAANDISHI NAMNA WALIVYOJIPANGA KUMENYANA KESHO..

Leave A Reply