The House of Favourite Newspapers

Essence ya Wiz Kid Yashika Nafasi ya Tisa Billboard

0

NGOMA ya ‘Essence’ wa msanii wa Nigeria Ayodeji Balogun  Wizkid, aliomshirikisha Terms imeshika nafasi ya 9 katika mtandao wa kimataifa wa Marekani wa Billboard Hot 100.

 

Essence iliingia katika kumi bora wiki iliyopita huku ikimfanya Wizkid kuwa Muafrika wa kwanza ambaye wimbo wake umeingia katika kumi bora katika mtandao huo.

 

Nafasi ya kwanza inashikiliwa na Lil Nas na Jack Harlow na wimbo wao wa ‘Industry Baby’, huku The Kid Laroi akimshirikisha Justin Bieber katika wimbo wa ‘Stay’ wakikamata nafasi ya 2, ‘Bad Habit’ ya Ed Sheeran inakimbiza nafasi ya 4 wakati Drake na wimbo wake wa ‘Way 2 Sexy’ ukikamata nafasi ya 5.

 

Billboard Hot 100 ni mtandao mkubwa wa muziki uliopo Marekani, unaopanga muziki kulingana na viwango vinavyotokana na mauzo ya muziki husika duniani na idadi kubwa ya watazamaji na wasikilizaji mitandaoni duniani kote.

Cc; @bakarimahundu

 

Leave A Reply