The House of Favourite Newspapers

Ester Kiama anaswa na ‘Serengeti Boy’

0

IMG20150317WA0032MSANII wa filamu Bongo, Ester Kiama.

Imelda mtema
MSANII wa filamu Bongo, Ester Kiama hivi karibuni alinaswa pande za Bahari Beach jijini Dar akijiachia na kiserengeti boy aliyejulikana kwa jina moja la Zuberi.

Chanzo kilimwaga ubuyu kuwa wawili hao walikuwa wamefika katika fukwe hizo kwa lengo la kuponda raha na mara nyingi walionekana wakitembea pamoja wakiwa wameshikana mikono huku wakizungumza na kuangua vicheko.

IMG-20160131-WA0008“Jamani huyu Ester yupo huku ufukweni na kijana mdogo-mdogo hivi, wanajiachia tu tena mara nyingi wanao-nekana wakicheka huku wakishikana mikono na kukumbatiana,” kilisema chanzo.

Showbiz Xtra baada ya kupata habari hizo, lilifanikiwa kunasa picha za tukio hilo kisha likamnyanyulia ‘waya’ Ester ambapo alikiri kuwepo na kijana huyo na kwamba ni mwanamuziki na wala hawana uhusiano wa kimapenzi bali walikuwa wakirekodi video ya muziki.

Leave A Reply