The House of Favourite Newspapers

Mwanafunzi Mtanzania Avamiwa, Adhalilishwa India

0

india (2)Gari la mwanafunzi raia wa Sudan likiteketezwa kwa moto.

Bangalore, India

MWANAFUNZI raia Mtanzania ameshambuliwa na kuvuliwa nguo na umati uliokuwa na hamaki katika jiji la Bangalore, Kusini mwa India.

Tukio hilo lilitokea Jumapili iliyopita majira ya usiku baada ya gari la mwanafunzi amabaye ni raia wa Sudan anayedaiwa kuwa alikuwa anaendesha gari huku amelewa, kumgonga na kumuua mwanamke mmoja aliyekuwa amelala pembezoni mwa barabara katika eneo hilo.

Polisi wameambia mwandishi wa BBC Hindi, Imran Qureshi mjini Bangalore kwamba, baada ya tukio hilo umati ulikusanyika eneo la Hessarghatta na kumshambulia mwanafunzi huyo Msudan kwa kumpiga na kisha gari lake kuteketezwa lakini alifanikiwa kutoroka.

india (1)

Eneo la tukio

“Dakika 30 baadaye, wanafunzi wanne (wote raia wa Tanzania), walikuwa wakipita eneo hilo, walisimama na kuuliza kilichotokea. Ndipo waliposhambuliwa,” Bernandoo Kafumu, rais wa chama cha wanafunzi wa Tanzania katika chuo kimoja huko India amesema.

Umati ulimvamia mwanafunzi huyo wa kike wenye umri wa miaka 21 pamoja na marafiki zake watatu, wote Watanzania.

Walikuwa wakipitia eneo hilo muda mfupi baada ya ajali kutokea. Umati ulimkimbiza mwanamke huyo na “kumvua blauzi”, polisi wamesema.

Ubalozi wa Tanzania umeitisha taarifa kuhusu kisa hicho, ripoti zinasema.

“Mwanamke huyo hata hakumfahamu mwanamume huyo (wa Sudan) aliyehusika katika ajali hiyo,” mwanachama wa chama hicho cha wanafunzi ambaye hakutaka kutajwa alisema.

 

Kisa hicho kilitokea usiku wa Jumapili, lakini kiliripotiwa mara ya kwanza Jumanne.

burnt_car

 

Gari la wanafunzi Watanzania likiwa limetekezwa kwa moto

“Baada yao kushambuliwa, Watanzania hao walikimbia hadi kwenye gari lao na kujaribu kutoroka. Lakini kulikuwa na kizuizi, na walishuka na kukimbia kwa miguu. Alikimbilia maisha yake. Wenyeji walimkimbiza na kumvua nguo,” ameongeza.

Watu hao pia waliteketeza gari hilo la Watanzania.

Afisa wa ngazi ya juu wa polisi amethibitisha kwamba “blauzi yake iliraruliwa na kuvuliwa, lakini hakunyanyaswa kingono”.

“Baada ya habari kutokea kwenye vyombo vya habari Jumatano, tulimuomba (mwanafunzi huyo) kuwasilisha rasmi malalamishi. Tunafuata taratibu zote, atachunguzwa na daktari,” TR Suresh, naibu kamishna wa polisi wa Bangalore kaskazini, ameambia BBC Hindi.

Bangalore, ina mamia ya wanafunzi wa kigeni, wakiwemo 150 kutoka Tanzania.

Watu wanne wanaotuhumiwa kuhusika katika tukio hilo wamekamatwa, shirika la habari la AP limeripoti.

Waziri wa mashauri ya kigeni wa India, Sushma Swaraj, aliandika kwenye Twitter kwamba amesikitishwa sana na “kisa hicho cha aibu” kilichotokea Jumapili eneo la Bangalore.

Bi Swaraj amesema polisi wamewakamata washukiwa wanne ambao watafunguliwa mashtaka.

Mji wa Bangalore ni kitovu cha teknolojia ya habari na mawasiliano nchini India.

Wanafunzi Waafrika mjini Bangalore wamesema wanaishi na hofu ya kushambuliwa.

Bw Bosco Kaweesi, mshauri wa kisheria wa Chama cha Wanafunzi kutoka Afrika, anasema wanafunzi wengine watatu wa kike kutoka Tanzania waliokuwa pamoja na mwanafunzi huyo garini pia walipigwa.

Gari lao liliteketezwa.

Kaweesi amesema huenda kisa hicho kilitendeka kimakosa, akisema gari la wanafunzi hao lilikuwa limefuata gari la mwanafunzi kutoka Sudan ambalo lilimgonga na kumuua mwanamke aliyekuwa amelala pembezoni mwa barabara.

Wanafunzi hao hawakumfahamu mwanafunzi huyo wa kiume aliyetoka Sudan, ambaye pia alipigwa na gari lake kuteketezwa.

Leave A Reply