The House of Favourite Newspapers

Ester Kiama kutolewa kizazi

0

DSC_3444Msanii wa filamu Bongo, Ester Kiama

Na Imelda Mtema
MASKINI! Msanii wa filamu Bongo, Ester Kiama, huenda akatolewa kizazi baada ya madaktari kugundua uvimbe mkubwa unaosababisha kupatwa na maumivu ya mara kwa mara.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi huku mwili wake ukionekana kupungua, Ester alisema amekuwa akipata maumivu makali ya tumbo kiasi ambacho wakati mwingine hupoteza fahamu kabisa kabla ya kuamua kwenda Hospitali ya Aga Khan kutibiwa.

“Jamani nilikuwa naumwa sana tumbo, lilikuwa linawaka moto kabisa kuna kipindi nashindwa kula, kulala wala kufanya chochote kile mpaka nilipoenda kuonana na mtaalamu, akaniambia nina uvimbe mkubwa sana kwenye kizazi changu,” alisema Ester.

“Yaani mimi nina mtoto mmoja tu na mipango yangu ilikuwa ni kuongeza wengine na nilikuwa napenda sana Mungu asaidie kama kuna njia nyingine itawezekana ili nisitolewe kizazi changu kwa kweli, kwani nitakuwa mpweke mno,” alisema Ester.

Leave A Reply