The House of Favourite Newspapers

Etihad Kuunganisha Abu Dhabi na Venice, Italia

0

Etihad-livery-7_Standard

Shirika la Ndege la Etihad katika nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu, linatarajia kupanua huduma za usafiri wa anga nchini Italia katika mji wa Venice kwa ndege ya kila siku kwenye Uwanja cha Ndege cha Marco Polo.

Huduma hiyo mpya itakayoanza tarehe 30 Oktoba, 2016 itatumia ndege aina ya Airbus A319, ikiwa na viti 16 kwa abiria wa daraja la kwanza na viti 90 kwa daraja la kawaida. Etihad, pamoja na mshirika wake Alitalia, watatumia jumla ya ndege 35 zitakazofanya safari zake ndani na nje ya Italia kwa wiki, ikiwamo safari za kwenda na kurudi Milan na Roma kila siku.

Etihad kupitia ndege yake ya kuelekea Venice pia itatoa huduma za haraka kwa wageni watakaosafiri kati ya nchi za Falme za Kiarabu na jiji la Italia. Huduma hizo mpya vilevile zitatumia ndege za moja kwa moja kwenda Sydney na Melbourne (Australia) pamoja na vituo muhimu vya mataifa yanayounda Shirikisho la Mabaraza ya Ghuba (GCC), Bara Hindi na Asia ya Kusini na Kaskazini kupitia Abu Dhabi.

Mji wa Venice umejirudishia hadhi yake kutokana na vivutio mbalimbali vilivyopo, kama vile madaraja na mifereji ambayo hutambulika kama vituo mashuhuri vya utalii duniani, wakati Italia ni nchi ya tano duniani kwa kutembelewa zaidi na wageni, ambapo kwa mujibu wa Shirika la Utalii duniani (UNWTO) nchi hiyo ilitembelewa na wageni wa kimataifa zaidi ya milioni 50 kwa mwaka 2015.

Shirika la ndege la Etihad lilianza kutoa huduma zake mjini Milan mwaka 2007, kabla ya jiji la Roma kuongezwa katika utaratibu huo mwaka 2014, hii ilichangia kuimarisha uhusiano wa kibiashara kwa mataifa ya Falme za Kiarabu na Italia. Biashara baina ya Falme za Kiarabu na Italia ilikua na kufikia kiasi cha dola za Kimarekani 6.14 bilioni mwaka 2015 na wizara ya uchumi katika Falme za Kiarabu ilisajili zaidi ya kampuni 90 za kiitali mwaka huo.

Afisa Mkuu wa Mipango na Mikakati wa Shirika la Ndege la Etihad, Kevin Knight amesema: “Kuanzisha huduma zetu kwenda Venice zimesaidia usafiri baina ya Italia na Abu Dhabi kwa kuongeza mtandao wa shirika letu unaoendelea kukua hadi kufika maeneo mbalimbali kama Australia. Washirika na wabia wetu Alitalia, kwa pamoja tunaimarisha uhusiano muhimu wa kibiashara baina ya Italia na Falme za Kiarabu (UAE)”.

Kwa sasa, Alitalia inashughulikia safari za Venice kwenda Abu Dhabi kwa kushirikiana na Shirika la Etihad. Pia imeamua kuhamishia ndege zake kwenye ratiba ya mtandao wake wa kimataifa itakayoanza katika msimu wa baridi mwaka 2016.

Ratiba ya Shirika la Ndege la Etihad kwa ndege ya Venisi- Marcopolo, itakayoanza rasmi tarehe 30 Oktoba, 2016

. Nambari ya ndege  

Eneo itokapo

 

Kuondoka

 

Eneo iendako

 

Kuwasili

 

Mzunguko

 

Aina ya ndege

EY79 Abu Dhabi (AUH) 0230 Venice Marco Polo (VCE) 0640 Daily

kilasiku

A319
EY80 Venice Marco Polo (VCE) 1055 Abu Dhabi (AUH) 1955 Daily

kilasiku

A319

 Muhimu: Safari zote zimezingatia muda katika eneo husika.

Kuhusu Shirika la Anga la Etihad

Idara ya Anga ya Etihad (EAG) inafanya shughuli zake maeneo mbalimbali duniani na idara ya usafirishaji imeundwa kwa sehemu nne ambazo ni Etihad, ambalo ni Shirika la Ndege  katika Mataifa ya Umoja wa Falme za Kiarabu, Etihad-Uhandisi, Idara ya Hala na Wanahisa. Shirika limewekeza sehemu katika mashirika saba ya ndege: AirBerlin, AirSerbia, Air Seychelles, Alitalia, jet Airways, Virgin Australia na kwa upande wa Uswisi ni Darwin Airline ambalo linafanyia biashara kama eneo la Etihad.

Kutoka makao makuu Abu Dhabi, Shirika la Etihad limetangaza mpango wa kuhudumia abiria 117 na vituo vya kusafirishia mizigo Mashariki ya Kati, Afrika, Ulaya, Asia, Australia na Marekani. Shirika hili lina jumla ya ndege aina ya Airbus 122 na Boeing pamoja na  ndege 204 zilizoagizwa na kampuni, zikiwamo Boeing787s zipatazo 71, Boeing777Xs zipatazo 25, Airbus A350s zipatazo 62 na AirbusA380s zipatazo 10. Kwa taarifa zaidi, tafadhali tembelea:www.etihad.com

Kwa mawasiliano zaidi:

Jonathan Hill

Oisa Mawasiliano wa Shirika la Etihad

simu:   +971 2 511 1539

Barua pepe:  [email protected]

Leave A Reply