The House of Favourite Newspapers

Etihad Yaungana na Mwanamitindo Maarufu India Katika Wiki ya Mitindo

0

Pic 1

Mbunifu maarufu wa India, Manish Malhotra (katikati) na Mkuu wa Shirikisho la Mawasiliano wa Shirika la Etihad Amina Taher (wa mwisho kushoto) wakiwa katika pozi mjini Mumbai kufuatia tangazo la ushirikiano wao kwa ajili ya wiki ya mitindo itakayofanyika wiki ijayo.

Pic 2

Manish Malhotra (katikati) na Amina Taher (kulia) wakiwa na mrembo katika tangazo la leo kuhusu ushirikiano wake na Shirika la Etihad katika wiki ya mitindo ya Lakme   inayotarajiwa  kuanza hivi karibuni. Habari zaidi kuhusu Etihad na wiki ya mitindo ya Lakme zinapatikana facebook katika @etihad.airways, katika Instagram @EtihadAirways na kupitia hashtag #RunwayToRunway

Shirika la Ndege la Etihad kwa kushirikiana na mbunifu wa mitindo Manish Malhotra aliyerudi upya kwenye fani hiyo, limeandaa maonyesho ya wabunifu yatayofanyika hivi karibuni katika wiki ya mitindo ya Lakmé mjini Mumbai.

Shirika hilo lilojishindia tuzo hivi karibuni litaungana na mbunifu huyo maarufu katika tukio kubwa la maonyesho hayo atakalolifungua katika mji mkuu wa kibiashara (Mumbai) wakati wa msimu wa baridi kuanzia agosti 24 hadi 28.

Manish Malhotra anajulikana kwa ubunifu wa mavazi na mapambo ya kifahari yanayotumiwa na nyota wengi wa filamu za Bollywood na sinema za Kihindi kwa zaidi ya miongo miwili, nbumifu huyo pia amekuwa kielelezo muhimu katika tasnia ya mitindo ulimwenguni.

Katika onyesho lake la usiku, lililopewa jana la ‘Etihad yamtambulisha Manish Malhotra, litakuwa ni tukio lenye msisimko wa pekee kwa watakaohudhuria kupata nafasi ya kumuona sehemu yoyote atakapokuwa siku hiyo au kumuona katika hafla itakayofuata baada ya hapo. Ni miezi michache imepita baada ya Shirika la Etihad kutumia teknolojia iliyoianzisha ili kuwapatia wateja fursa ya kipekee, kuonana moja kwa moja na muigizaji maarufu wa kike Nicole Kidman kutoka Hollywood ndani ya ndege ya shirika hilo aina ya Airbus A380 ambayo imepokea tuzo.

Ushirikiano wa shirika la Etihad na Manish Malhotra ni jitihada mpya zinazofanywa na shirika letu kwa upande wa Abu Dhabi kufuatia ufadhili wake katika tasnia ya mitindo, ikiwa ni juhudi za kulifanya shirika hili litumike katika tasnia hiyo. Hii itasaidia kuinua tozo za bidhaa za shirika na kuzipa thamani ya juu ulimwenguni.

Mapema mwaka huu, Shirika la Etihad limeingia katika makubaliano ya kidunia na kampuni inayojihusisha na uwakala wa mambo ya burudani (WME| IMG) kama mshirika endelevu wa tasnia ya mitindo, ambayo inaunganisha shirika la ndege na maeneo muhimu yanayojihusisha na fani ya mitindo ulimwenguni. Makubaliano haya ni yakwanza kuhusisha mataifa mbalimbali, ufadhili wa shirika katika miaka tofauti tofauti unasaidia kuinua tasnia ya mitindo.

Mumbai ni kituo kipya katika ufadhili wa mitindo ulimwenguni kutoka Shirika la Etihad, linalosaidia maonyesho 17 ya kila wiki jijini London, Milan, Sydney, New York na Mumbai, duniani kote kila mwaka. Huu ni mwendelezo kutoka katika ushiriki wa Etihad katika wiki ya mitindo ya Mercedes-Benz Berlin na wiki ya mitindo Mercedes-Benz Australia.

Ushirikiano na Manish Malhotra, umetangazwa leo Mumbai katika mkutano wa vyombo vya habari uliohusisha uoneshaji wa bidhaa zake mpya, ni onesho la pili ambalo linashirikisha  mbunifu na shirika la Etihad baada ya kufanikiwa katika ushirika wake na jumba la mitindo la The Oscar de la Renta katika msimu huu wa joto.

Patric Pierce, makamu wa rais katika ufadhili kwenye shirika la Etihad, amesema, “Tasnia ya mitindo na shirika la Etihad inawakilisha ubora wa bidhaa na sifa ya pamoja ya kuwa na ari ya ubunifu na uvumbuzi ikiwa kama muongozo mkuu unaoakisi huduma zetu mpya za ndani pamoja na ukarimu wetu.

“Kwa hiyo tumefurahi kushirikiana na Manish Malhotra, moja ya wabunifu wa India ambaye anapendwa sana, kwa ufunguzi wa tukio lake la wiki ya mitindo ya Lakḿe. Litakuwa ni tukio lisiloweza kusahaulika litakalo husisha teknolojia ileile ya VR ambayo tuliizinduainayopatikana  kwenye ndege ya A380.

Akizungumza na vyombo vya habari, Manish Mahotra alisema “Nimefurahishwa kuwa mshirika wa Etihad kwakuwa sasa pande mbili zenye malengo zimekutanishwa. Hili itakuwa ni onyesho la kwanza kabisa ambalo litawapa watazamaji uzoefu usio na kikomo pamoja na nafasi.”

Neerja Bhatia, Makamu wa Rais wa Shirika la Ndege la Etihad katika Bara Hindi anaongeza: “Shirika la Etihad ni mshirika mkubwa wa India ambae ana mtandao mpana wa kimataifa unao iunganisha India na dunia, akiwamo mshirika wetu wa kimkakati Jet Airways. Pamoja na tuzo yetu iliyotokana na ndege ya A380 ambayo imetambulishwa katika safari za Mumbai- Abu Dhabi hivi karibuni iliyotengenezwa kwa muonekano wa kipekee wa vyumba vitatu maalumu vya makazi ukiwa hewani, muonekano huu  mahususi umetokana na tasnia ya mitindo.”

“Shirika la Etihad limedhamiria kuunganisha maeneo yote ya ubunifu, uvumbuzi na mitindo ili kuja kuwa shirika lenye mtindo wa pekee kabisa wa maisha. Huduma zetu katika A380 kutoka Mumbai kwenda Abu Dhabi na kuendelea kuelekea Amerika, hazina kikomo wakati wa kuingia na kutoka katika miji hii inayojihusisha na mitindo pale unaposafiri na ndege zetu za hadhi ya juu.

Wiki ya mitindo ya Lakme ni mshirika mkuu wa pili wa Etihad nchini India kufuatia ufadhili wake wa Wahindi wa Mumbai, moja ya timu za kriketi iliyofanikiwa sana katika ligi kuu ya India wakiwa kama wadau wetu muhimu.

KUHUSU IDARA YA ANGA YA ETIHAD

Idara ya Anga ya Etihad (EAG) imesambazwa katika maeneo mbalimbali duniani na idara ya usafirishaji imeundwa kwa sehemu nne ambazo ni Etihad, Shirika la ndege la Etihad ambalo ni shirika la taifa katika Umoja wa falme za za Kiarabu, Etihad-uhandisi, idara ya Hala na wanahisa. Idara imewekeza sehemu ndogo katika mashirika saba ya ndege: AirBerlin, AirSerbia, Air Seychelles, Alitalia, jet Airways, Virgin Australia na kwa upande wa Uswisi ni Darwin Airline ambalo linafanyia biashara kama eneo la Etihad

Kutoka katika kambi ya Abu Dhabi, shirika la Etihad limetangaza mpango wa kuhudumia abiria 117 na vituo vya kusafirishia mizigo Mashariki ya kati, Afrika, Ulaya, Asia, Australia na Marekani. Shirika hili lina jumla ya ndege aina ya Airbus 122 na Boeing pamoja na  ndege 204 zilizoagizwa na kampuni, zikiwamo Boeing787s zipatazo 71, Boeing777Xs zipatazo 25, Airbus A350s zipatazo 62 na AirbusA380s zipatazo 10. Kwa taarifa zaidi, tafadhali tembelea: www.etihad.com

Kuhusu Manish Malhotra

Zaidi ya miaka 26 iliyopita, Manish Malhotra ameibadilisha tasnia ya mitindo, kwanza kupitia kazi yake katika sinema ya Kihindi na zaidi ya miaka 11 iliyopita akitumia kibandiko cha kitamaduni kilichokuwa na nembo ya MANISH MALHOTRA. Kibandiko kilikuwa kinawiana na mapambo ya kifahari yatumikayo katika mavazi ya kisasa sehsmu za Mumbai, Delhi, Dubai na miji mingine.

Mwaka 2013 hadi 2014 chapa ilienea duniani ikijipambanua kwa alama ya mkanyago wa binadamu kupitia www.manishmalhotra.in chapa hiyo iliikgiza zaidi ya rupia bilioni1 na kuifanya kuwa moja ya nyumba za kifahari katika tasnia ya mitindo kufikia hatua hiyo. Manish pia ni mmoja wa wa wanamitindo wenye ushawishi mkubwa nchini India ambaye anawafuasi 1.4 milioni katika Instagram na wafuasi 1.7 katika akaunti yake ya twitter. Hadithi ya ubunifu wa nembo yake  imechochewa na haja ya wateja wa Manish kutaka kufufua sanaa ya mikono nchini india.

Kuhusu wiki ya mitindo ya Lakme

Wiki ya mitindo ya Lakme imeandaliwa kwa ushirikiano wa Lakme, chapa namba moja katika vipodozi na urembo nchini India, pamoja na IMG Reliance Pvt. Ltd.,viongozi katika michezo, mitindo na burudani, masoko na utawala, tukio hili limebuniwa likiwa na mtazamo wa “kuendeleza mitindo na kuiunganisha India katika ulimwengu wa mitindo” Wiki ya mitindo ya Lakme linaandaliwa mara mbili kila mwaka, kwa mwaka 2016 maonyesho haya yatafanyika kuanzia Agosti24 mpaka Agosti 28 huko St. Regis Mumbai. Kwa taarifa Zaidi tembelea http://www.Lakmefashionweek.co.in

Kwa taarifa zaidi wasiliana na:

Updesh Kapur

Ofisa Mawasiliano wa Shirika la Ndege la Etihad

: +971 2 511 3276

simu:   +971 5 6546 1402

baruapepe:  [email protected]

 

Leave A Reply