The House of Favourite Newspapers

EWURA Yasitisha Bei Mpya za Mafuta Nchini

0

MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza kusitishwa kwa bei mpya za mafuta zilizotangazwa ambazo zilipaswa kuanza kutumika  Septemba 1, 2021.

Serikali imesitisha bei za mafuta zilizoanza kutumika leo Septemba 2, 2021 kote nchini na kuunda timu ya kuchunguza na kuangalia viashiria vinavyofanya kupanda kwa bei.

 

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Godfrey Chibulunje amesema, “Serikali imeunda Timu Maalum kwa ajili ya kuangalia bei zinavyopangwa na viashiria mbalimbali vinavyosababisha bei iendelee kupanda.

 

Ameongeza, “Bei za zamani zitaendelea kutumika mpaka pale Timu Maalum ambayo imeundwa na Serikali kupitia na kutoa majibu”

Mafuta hayo yamepanda ikiwa ni miezi miwili tangu yalipopanda kwa mara ya mwisho Julai Mosi 2021 bei ambayo ilianza kulalamikiwa. Mwaka huu ni mara ya tatu kupanda bei za mafuta mara ya kwanza ilikuwa Aprili.

BEI MPYA ZA MAFUTA ZILIKUWA HIVI CHINI HAPA

Leave A Reply