The House of Favourite Newspapers

Ex-Wife Wa Ben Pol Alipuka- “Nilimwacha Mwanaume, Kisa Mchafu Jikoni”

0
Anerlisa Muigai ni mrembo au sosholaiti maarufu wa nchini Kenya.

Anerlisa Muigai ni mrembo au sosholaiti maarufu wa nchini Kenya ambaye amekuwa maarufu nchini Tanzania baada ya miaka kadhaa kuolewa na msanii wa Bongo Fleva, Ben Pol kisha wakatalikiana hivyo anabaki kuwa EX-Wife wa staa huyo wa RnB.
Habari mpya ni kwamba, mrembo huyo ambaye hakubahatika kupata mtoto na Ben Pol ambaye pia ni mfanyabishara mkubwa ameibuka na jipya akisema kuwa, aliwahi kumuacha mwanaume kisa alikuwa mchafu jikoni.
Anerlisa amefunguka hayo wakati akijibu moja ya video iliyopostiwa kwenye Instagram ikimuonesha mwanaume ambaye hajasafisha jiko.
Anerlisa alijibu video hiyo kwa emoji ya kucheka akisema aliwahi kumuacha mwanaume ambaye alikuwa na tabia ya uchafu kama hiyo.
Jibu hilo la Anerlisa limeibua maswali na sintofahamu kwamba huwenda anayezungumziwa ni Ben Pol kwa sababu ndiye EX-Husband wake anayefahamika zaidi.

STORI NA SIFAEL PAUL, GPL

STEVE NYERERE amuwashia moto BABU TALE AJIUZULU huo UDAKTARI, amshukuru SPIKA DKT TULIA AKSON..

Leave A Reply