The House of Favourite Newspapers

EXCLUSIVE: DANZAK Afunguka Kusainiwa WCB, DIAMOND Anamchukua? – VIDEO

Bila shaka jina la Danzak litakuwa sio geni masikioni mwako, kufuatia stori yake iliyowavuta wengi ya kuukacha Urubani na kujikita kwenye muziki na kuachia ngoma yake ya falling na sasahivi ameachia wimbo mpya unaoitwa Kichaa.

Danzak amepiga stori na Global TV na kufungukia suala la kusainiwa kwenye lebo kubwa ya muziki WCB inayomilikiwa na mtu mzima Diamond Platnumz, ambapo amesema ikitokea akapata fursa hawezi kukataa kwani ni neema.

Danzak pia ameulizwa kuhusiana na kufanya video yake ya Kichaa Bongo na Director Kenny, kwani video ya kwanza ameshuti na Justin Campus wa Afrika Kusini, ambapo amesema kwa sasa ameamua kufanya kazi na watu wa nyumbani na si kutoa fursa tu kwa ma director wa nje kwani ana amini hata Bongo wapo wanaoweza kufanya vizuri kama Kenny.

Comments are closed.