The House of Favourite Newspapers

Harusi Ya LULU Makonda Afunguka, Amtaja Diamond na Lemutuz! – VIDEO

Hivi karibuni kumekua na Fununu za hapa na pale kuhusu ndoa ya Lulu pamoja na Majizo ambayo ingefungwa mwezi wa kumi na mbili mwaka jana lakini ikawa kimya.

kupitia ukurasa wake wa instagram, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Harusi Hiyo, Paul Makonda, amezua gumzo baada ya kuposti kipande cha video inayomuonesha Mc Pilipili akiwa anamvalisha pete mpenzi wake anayejulikana kwa jina la Mena na kuambatanisha na ujumbe mzito.

“Sipati picha wale waliotuacha wanavyokutazama. Mmoja eti anasema unaigiza. Nakuomba mc Pilipili umsaidie na Diamond Platnumz, kwani yeye kila tarehe ikikaribia anasogeza mbele ona sasa anamsubiri Rick Ross aje, sasa sijui ni harusi au Tamasha, heri ya Majizzo, ameamua kufungia China sasa tunasubiri send off huku, balaa lipo kwa Lemutuz,  kila siku anaachwa yaani kimsingi mji huu ndio pekee watu wanaanza Honey moon kabla ya kufunga Ndoa”

Kufuatia Posti hiyo Makonda amewaacha watu njia panda kuwa Ndoa  ya Lulu na Majizzo inayosubiriwa kwa hamu kumbe imeshafungwa nchini China na kwa sasa ni Mume na Mke Halali.

 

Comments are closed.