The House of Favourite Newspapers

EXCLUSIVE: GLOBAL TV ONLINE YATUNUKIWA ‘GOLD CREATOR AWARD’ NA YOUTUBE – (PICHAZ)

Mkurugenzi wa Makampuni ya Global Group, Eric Shigongo akiikumbatia Gold Creator Award kwa furaha mara baada ya kukabidhiwa.

CHANNEL namba moja ya mtandaoni Afrika Mashariki kwa burudani, habari za jamii, kitaifa, kimataifa, Siasa na michezo na breaking news, Global TV Online imetunukiwa ‘Gold Creator Award‘ na wamiliki wa mtandao maarufu wa video duniani, YouTube.

Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho,  akiipokea kwa furaha Gold Creator Award kutoka YouTube.

Ni kawaida ya mtandao wa YouTube kutambua channel zake zote zenye mchango mkubwa kwa jamii kupitia video mbalimbali zinazowekwa kwenye mtandao huo.

Mhaririri Mtendaji wa Global Publishers, Saleh Ally,  akiifurahia tuzo hiyo.

Video hizi zinaweza kuwa za kitu chohote kinachofurahisha, kuelimisha, na kuiburudhisha jamii nzima ya wana-YouTube ambao ni watazamaji kutoka kila pembe ya dunia.

 

Shigongo na Saleh ‘full’ vicheko.

Kwenye list ya zile channel zinazoleta impact hiyo, channel yako pendwa ya Global TV Online imepata bahati ya kuwa miongoni mwa channel hizo, hivyo kufanikiwa kujinyakulia zawadi ya ‘YouTube Gold Play Button’ kutoka makao makuu ya YouTube, San Bruno, California, nchini Marekani kwa kujikusanyia Subscribers (watazamaji waliojiunga) zaidi ya milioni moja (1,000,000) ambapo kwa sasa ina Subscribers zaidi ya 1,236,000.

Shigongo akizungumza na wafanyakazi wenzake  (hawapo pichani).

Tuzo hiyo imekabidhiwa leo Desemba 20, 2018 kwa Mkurugenzi wa Makampuni ya Global Group yanayomiliki Global TV Online, Eric Shigongo,  kwenye Ofisi za Global Publishers zilizopo Sinza-Mori, jijini Dar es Salaam.

Wafanyakazi wa Global Group wakimsikiliza Shigongo.

 

Akizungumza na wafanyakazi wa Global Group mara baada ya kupokea tuzo hiyo, Shigongo ameipongeza timu ya Global TV na wafanyakazi wote kwa mchango na kujituma kwao.

Amewataka kuhakikisha wanazalisha habari bora, kwa wakati na za kweli ili kuendelea kuuhabarisha umma wa Tanzania na dunia nzima.

Timu ya Global TV Online ikiwa katika kilele cha furaha.

Aidha, Shigongo amewashukuru YouTube kwa kutambua mchango wa Global TV katika kuihabarisha jamii huku akiwapa pongezi kubwa mashabiki (watazamaji na subscribers wa Global TV ambao wamekuwa wakifuatilia habari zake kwani bila wao tuzo hii isingepatikana.

Shigongo akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo.

Shigongo, amewataka mashabiki na watazamaji kuendelea kuiamini na kuifuatilia Global TV na muda wote kwani ndiyo channel bora ya mtandaoni inayoongoza kwa sasa Afrika Mashariki.

…Mhariri mwandamizi wa Global Publishers, Elvan Stambuli,  akiwa na waandishi Imelda Mtema (kulia), Hamida Hassan, Eric Evarist na Msanifu Video, Kelvin.

Katika hatua nyingine, Shigongo amewatakia kila la heri wafanyakazi wake wote katika kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka (Krismasi na Mwaka Mpya).

Shigongo akizungumza na wafanyakazi wake.

Machi mwaka  jana 2017, Global TV Online ilitunukiwa tuzo ya kwanza na YouTube kwa kufikisha subscribers zaidi ya 1,000,000, jambo ambalo liliamsha mori kwa watangazaji, producers na uongozi wote wa Global TV online kuhakikisha wanatengeneza kazi bora zaidi, na leo ikiwa ni takribani miezi 21, Global TV online imepata tuzo nyingine ya pili kwa kufikisha zaidi ya subscribers milioni moja.

Shigongo akimpongeza Mrisho kwa kazi nzuri anayoifanya ya kusimamia kazi zote za kampuni.

YouTube hutoa  Play Buttons hizi kwa stage nne ambazo ni:

  • The Silver Play Button, kwa channel zilizofikia subscribers 100,000.
  • The Gold Play Button, kwa channel zilizofikia subscribers 1,000,000.
  • The Diamond Play Button, kwa channel zilizofikia subscribers 10,000,000.
  • The Ruby Play Button, kwa channel zilizofikia subscribers 50,000,000.
Watangazaji, Asma na Anna Mbawala wakiwa na tuzo.

 

…Kelvin na mwandishi, Aziz Hashim.

 

Wahariri wa Gazeti la Amani, Erick Evarist na Joseph Shaluwa.

 

Kiongozi wa Kitengo cha TEHAMA, Edwin Lindege na Stambuli.

 

Mhariri wa Gazeti la Ijumaa Wikienda, Sifael Paul.

 

Mtangazaji wa Michezo wa Global TV Online, Aaron Felix.

 

Mrisho, Shigongo, Mtangazaji wa global TV, Felister Massae na Saleh.

 

Shigongo, YouTube Manager wa Global TV, Isri Mohammed na Saleh.

 

Shigongo, mtangazaji wa Global TV, Catherine Kahabi na Saleh.

 

Timu ya Global TV wakifurahia kwa pamoja.

 

PICHA NA MUSA MATEJA | GLOBAL TV ONLINE

Comments are closed.