visa

Exim Bank Yachangia Mil. 25 Vitanda vya Wanafunzi Arusha

 Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Tanzania, Jaffari Matundu (wa tatu kulia) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Sh milioni 25  kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (wa tatu kushoto) ikiwa ni mchango wa benki hiyo kwa ajili ya ununuzi wa vitanda pacha (double deckers) 47 vya hosteli ya wanafunzi wa Shule mpya ya Sekondari ya Mrisho Gambo iliyopo mkoani Arusha. Wengine ni pamoja na maofisa waandamizi kutoka mkoa wa Arusha pamoja na benki hiyo.

 

Benki ya Exim Tanzania imechangia kiasi cha Sh milioni 25 kwa ajili ya ununuzi wa vitanda pacha (double deckers) 47 vya hosteli ya wanafunzi wa Shule mpya ya Sekondari ya Mrisho Gambo iliyopo mkoani Arusha.

 

Hatua hiyo ni muendelezo wa benki hiyo katika kuunga mkono jitihada za serikali katika kuboresha sekta ya elimu hapa nchini.

 

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada huo iliyoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Tanzania, Jaffari Matundu alisema, mchango huo ni sehemu ya Mpango wa Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) unaotekelezwa na benki hiyo ukifahamika kwa jina “Exim Cares” ukilenga kusaidia jamii.

 

Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dk. Maulid Suleiman Madeni (katikati) akifafanua jambo kuhusu maendeleo ya elimu katika mkoa huo kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Tanzania, Jaffari Matundu (wa pili kulia) pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Arusha (RC), Mrisho Gambo (kulia kwake)  wakati benki hiyo ilipokabidhi fedha kiasi cha Sh milioni 25-  kwa ajili ya ununuzi wa vitanda pacha (double deckers) 47 vya hosteli ya wanafunzi wa Shule mpya ya Sekondari ya Mrisho Gambo iliyopo mkoani Arusha.

 

“Benki ya Exim tunaamini kuwa tunalo jukumu kubwa la kufanya katika kuwezesha mabadiliko chanya katika jamii zinazotuzunguka. Elimu ni kati ya maeneo yetu ya kuzingatia na mpango huu unaendana na mkakati wetu wa kubadilisha maisha ya wanafunzi chini ya mpango wa  ‘Exim Cares’ kupitia vitendo endelevu.’’ Alisema.

 

“Benki ya Exim tunavutiwa zaidi katika kuleta athari chanya kwenye jamii ambazo tunatoa huduma zetu, hivyo kwa kuangalia nafasi yetu tumeaona kwamba kwenye hili tunaweza kusaidia vitanda pacha vipatavyo 47 vikiwa na uwezo wa kubeba wanafunzi zaidi ya 100.’’

 

Alitoa wito kwa taasisi na wadau mbalimbali nchini kuhakikisha wanawekeza kwenye uwezeshaji wa vijana kupitia elimu kutokana na ukweli kuwa bado wanakabiliwa na changamoto nyingi.

 

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (wa pili kushoto) akiongoza timu ya viongozi waandamizi wa mkoa wa Arusha akiwemo Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dk. Maulid Suleiman Madeni (Kulia kwake) pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Tanzania, Jaffari Matundu (wa pili kushoto)  kukagua maendeleo ya ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari ya Mrisho Gambo iliyopo mkoani Arusha.

 

 

“Tumebaini kuwa kuna changamoto zinazoathiri vijana wa leo hususani wanafunzi ambazo zinaweza kuwaongoza kuelekea kwenye tabia zisizokubalika ndani ya jamii. Benki ya Exim, tunaamini kwamba kuna haja ya kuelekeza umakini na kuzingatia uwezeshaji wa vijana kupitia elimu. Tutaendelea kuwekeza katika hili na kutimiza wajibu wetu kwa miaka mingi ijayo,” alisema.

 

Akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo, Gambo aliipongeza benki hiyo lwa msaada huo huku akibainisha kuwa umetolewa kwa wakati muafaka.

 

“Kupitia msaada huu kutoka benki ya Exim tutaweza kuwasaidia wanafunzi wetu kukaa hosteli, hasa wale ambao kwa sasa wanatembea umbali mrefu kwenda na kurudi. Kwa kweli kupitia msaada huu msaada huu utawawezesha kujifunza vizuri na kutambua ndoto zao za masomo, ” alisema Gambo.

 

Alizidi kusema kuwa mahitaji ya mradi huo ni vitanda 100 (Double Deckers) na godoro ambazo zitagharimu Shs milioni 53.7.
Toa comment