The House of Favourite Newspapers

Eymael: Kwa Ratiba Hii, Tukaze Sana

0

MBELGIJI Luc Eymael wa Yanga, ameichungulia ratiba yao ya mzunguko wa pili itakavyokuwa, akavuta pumzi kisha akaweka neno moja tu kwamba wanatakiwa kukaza.

 

Kocha huyo amesema kwamba ratiba hiyo ambayo wataicheza mechi 19 za ligi katika kipindi cha miezi mitatu itakuwa ngumu sana kwao ambapo watakuwa wanacheza kila baada ya siku tatu.

 

Yanga kwa sasa wamebakisha mechi moja kabla ya kumaliza mzunguko wa kwanza, kisha kuanza mzunguko wa pili ambapo watacheza na Prisons Februari 15 jijini Dar.

Akizungumza na Spoti Xtra, Eymael amesema; “Kwa sasa tunamaliza mechi zetu za mzunguko huu wa kwanza na tunataka kumaliza katika nafasi nzuri, lakini hesabu zilizopo ni katika mzunguko ujao.

 

“Mzunguko huo utakuwa na mechi kila baada ya siku kadhaa kwa hiyo cha kufanya ni kuhakikisha kwamba tunapambana kupata pointi katika kila mchezo kwa ajili ya kufanikisha kutimiza kile ambacho tumejiwekea kama timu.”

Leave A Reply