The House of Favourite Newspapers

Eymael: Simba Tulieni Dozi Yenu Ipo Tayari

0

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mbelgiji, Luc Eymael ameibuka na kusema kuwa hana presha na Simba kuwafuata katika Hatua ya Nusu Fainali ya Kombe la FA kwa kuwa tayari ameshawaandalia dawa.

 

Mbelgiji huyo ametoa kauli hiyo muda mchache baada ya Simba kuifunga Azam FC mabao 2-0 katika mchezo wa Kombe la FA uliopigwa juzi Jumatano kwenye Uwanja wa Taifa, Dar ambapo nusu fainali ya wababe hao inatarajiwa kupigwa Julai 12, mwaka huu.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Eymael alisema upande wao hawana presha juu ya Simba kutinga hatua ya nusu fainali kwani anaamini ni moja kati ya mechi zitakazokuwa nyepesi kwake kutokana na wachezaji wake kuwataka wapinzani wao hao kila wakati.

“Sasa hivi malengo yetu yapo kwenye ligi kwa sababu mechi iliyo mbele yetu kubwa ni dhidi ya Kagera kwa sababu ni moja kati ya timu ngumu, tunachokiangalia ni kuona tunapata matokeo kwenye mchezo huo, hilo ndilo jambo kubwa kwetu.

 

“Sina presha juu ya Simba kuingia hatua ya nusu fainali kwa sababu kila kitu kwetu kipo sawa kwa sababu nahitaji kuendeleza rekodi dhidi yao, najua mechi kubwa ambayo imekuwa ikivuta hisia za wengi lakini hata wachezaji wenyewe wamefurahi na wanashukuru kwamba tunaenda kucheza na Simba kwenye hatua hiyo,” alisema Eymael.

Stori: Ibrahim Mussa, Dar es Salaam

Leave A Reply