The House of Favourite Newspapers

Ezden Jumanne: Ndoa yangu na Dida imenifunza mengi

0

1eziden (3)

Mtangazaji wa Runinga ya TV1, Ezden Jumanne kabla ya kufanya mahojiano Global TV akitabasamu.

1eziden (1)

…Akijibu maswali ya wafanyakazi (hawapo pichani) wa Global Publishers kupitia Global TV Online.

1eziden (4)

…Akiwa amepozi baada ya kumaliza mahojiano.

_PL_0419 _PL_0426 _PL_0436 _PL_0441

Wafanyakazi wa Global Publishers wakiwa katika mapozi mbalimbali na Ezden Jumanne.

MTANGAZAJI maarufu wa Kipindi cha One Show kinachoruka hewani kupitia Runinga ya TV1, Ezden Jumanne, amefungukia ndoa na aliyekuwa mke wake, Khadija Shaibu ‘Dida’ kuwa imemfunza mengi.

Akizungumza na Global TV Online leo katika mahojiano na Kipindi cha Exclusive, Ezden alisema kuwa katika siasa kuna kipindi mtu hufikia hatua ya kutoka ubunge na kuwa rais na ndivyo ilivyokuwa kwake kwani alikuwa amefikia hatua ya juu lakini kitendo cha kuachana kilimpa wakati mgumu sana.

“Sipendi kulizungumzia sana hilo kifupi nilikuwa katika wakati mgumu ambapo leo hii nimejifunza mengi kupitia maisha ya ndoa hasa pale mtu anapopenda sana,” alisema Ezden.

Mbali na ndoa yake hiyo iliyovunjika, Ezden alisema kuwa kwa sasa yupo katika uhusiano na mwanamke mwingine lakini hakupenda kumuanika hadharani kwa sasa.

Mahojiano kamili yatapatikana hivi karibuni kupitia www.globaltvtz.com

(PICHA: GLOBAL TV ONLINE)

Leave A Reply