The House of Favourite Newspapers

Fabrice Ngoma Aipa Jeuri Simba, Ahmed Ally Atamba ni wa Kipekee

0
Kiungo wao mpya, Fabrice Ngoma (katikati).

WAKATI Simba wakiwa nchini Uturuki kwenye maandalizi ya msimu ujao wa 2023/24, taarifa njema ni kuhusiana na kiungo wao mpya, Fabrice Ngoma ambaye unaambiwa anawapa jeuri mabosi na mashabiki wa timu hiyo kutokana na aina yake ya uchezaji katika eneo la kiungo.

Ngoma ambaye amepita katika klabu kubwa Afrika ikiwemo AS Vita ya DR Congo, Raja Casablanca (Morocco) na Al Hilal (Sudan), kwa sasa ni mali ya Simba kutokana na kusaini mkataba hivi karibuni.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally ameliambia Spoti Xtra kuwa, aina ya uchezaji wa Ngoma ni wa kipekee na ndani ya kikosi chao utawaongezea ubunifu mkubwa uliokosekana katika maeneo ambayo anacheza, hivyo wanatarajia makubwa zaidi kutoka kwake.

“Ngoma ana staili yake ya pekee ya kucheza soka, uchezaji wake umekosekana ndani ya Simba kwa maana ya kuwa kiungo wa chini kisha akawa na uwezo mzuri pia wa kushambulia na kufunga, hiyo kwetu haikuwepo, hivyo kwa ujio wake niwaambie tu wanasimba watafurahia zaidi.

“Sio tu Ngoma, wachezaji wote ambao tumewasajili ni wachezaji bora ambao watatufanya watupeleke katika nchi ya ahadi kwa kuwa naamini kila ambaye tumemsajili kipindi hiki ni mchezaji bora na ana uwezo mkubwa sana,” alisema kiongozi huyo.

STORI NA MARCO MZUMBE, SPOTI XTRA

”NYUMBANI KWANGU UKOKO HAUTUPWI, PESA HAITAFUTWI INAVUTWA” – MC LUVANDA AFUNGUKA| HARD TALK

Leave A Reply