The House of Favourite Newspapers

FAHAMU MADHARA YA UGONJWA WA VIDONDA VYA TUMBO

UGONJWA wa vidonda vya tumbo hutokea iwapo kidonda cha ukubwa wa angalau wa nusu sentimita kitatokea kwenye sehemu yoyote ya ukuta wa tumbo au utumbo wa binadamu.  Kwa kawaida tatizo hili huleta maumivu makali sana ya tumbo ingawa si lazima kila maumivu ayapatayo mgonjwa husababishwa na vidonda vya tumbo. Tafiti zimeonesha kwamba karibu asilimia 70 mpaka 90 ya vidonda vya tumbo husababishwa na aina ya vimelea vya bakteria wajulikanao kama Helicobacter pylori. Aidha, matumizi ya baadhi ya dawa za kutuliza maumivu za jamii ya Non Steroid Anti-inflamatory Drugs kama aspirin au diclofenac huweza kusababisha au kuongeza uwezekano wa kupata ugonjwa huu.

Kuna dhana iliyozoeleka kuwa vidonda vya tumbo huathiri zaidi mfuko wa kuhifadhia chakula yaani tumbo (stomach). Dhana hii si kweli kwani sehemu inayoathiriwa zaidi na tatizo hili ni sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo ijulikanayo kama duodenum.

Kuna makundi makuu yafuatayo ya ugonjwa huu: Vidonda vinavyotokea kwenye mfuko wa kuhifadhia chakula yaani tumbo kitaalamu Gastric ulcers, vidonda vinavyotokea kwenye sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo (Duodenal Ulcers), vidonda vinavyotokea kwenye koo (Oesophageal ulcers), vidonda vijulikanavyo kama Merckel’s diverticulum ulcers.

Vidonda vya tumbo husababishwa na mambo yafuatayo:

1.Maambukizi ya bakteria aina ya Helicobacter pylori

Imeonekana kuwa zaidi ya asilimia 50 ya watu duniani wana vimelea hivi katika utumbo. Aidha, miongoni mwao, karibu asilimia 80 huwa hawaoneshi dalili yoyote ya kuugua ugonjwa wa vidonda vya tumbo. Aina hii ya vimelea vya bakteria husababisha karibu asilimia 60 ya vidonda vinavyotokea kwenye tumbo (gastric ulcers) na zaidi ya asilimia 90 mwanzo wa utumbo (duodenal ulcers). Hali hii husababishwa zaidi na kushindwa kwa mfumo wa kinga mwilini kuwaua na kuondoa kabisa vimelea hawa ndani ya mwili.

Matokeo ya kushindwa huku husababisha kuwepo kwa maambukizi ya kudumu katika kuta za tumbo (chronic active gastritis), maambukizi ambayo huharibu mfumo na uwezo wa kuta za tumbo kutunza homoni/ kichocheo aina ya Gastrin, ambacho ni muhimu katika kuhakikisha mazingira ya tumbo yanakuwa na kiwango salama cha tindikali.

Kwa kawaida, kazi ya gastrin ni kuchochea utolewaji wa tindikali (gastric acid) kutoka kwenye seli za ukuta wa tumbo zijulikanazo kama Parietal cells. Iwapo bakteria hawa watashambulia na kuharibu ukuta wa tumbo, mfumo wa gastrin pia huharibika na hivyo kusababisha gastrin kuzalishwa kwa wingi hali ambayo pia huchochea uzalishaji wa gastric acid kwa wingi. Matokeo ya kuzalishwa kwa wingi kwa tindikali hii husababisha kuchubuka kwa ukuta wa tumbo na hivyo kusababisha vidonda vya tumbo.

2.Matumizi ya muda mrefu ya dawa za kuondoa maumivu

Ukuta wa utumbo hujilinda na madhara yatokanayo na tindikali ya utumbo (gastric acid) kwa kuwa na utando laini (mucus) ambao hutolewa na vichocheo vijulikavyo kama Prostaglandins. Dawa hizi za kundi la NSAIDs huharibu mfumo wa kutengeneza vichocheo hivi yaani prostaglandins na hivyo kufanya kuta za tumbo kukosa utando wa kuzilinda na mashambulizi ya tindikali hali ambayo husababisha kutokea kwa vidonda vya tumbo.

3.Uvutaji wa sigara

Uvutaj i sigara sambamba na maambukizi ya bakteria aina ya Helicobacter pylori huongeza madhara ya ugonjwa wa vidonda vya tumbo. Ifahamike tu kuwa uvutaji sigara pekee hausababishi vidonda vya tumbo.

4.Watu walio katika kundi la damu la O

Imeonekana pia kwamba kundi la damu lijulikanalo kama blood group O, halina uhusiano wa kusababisha vidonda vya tumbo.

5.Unywaji wa pombe

U n y w a j i w a p omb e p e k e e hausababishi vidonda vya tumbo. Hata hivyo, unywaji wa pombe sambamba na maambukizi ya vimelea vya Helicobacter pylori huongeza madhara ya ugonjwa wa vidonda vya tumbo. Vitu vinavyohusishwa na uongezaji wa madhara ya vidonda vya tumbo ni pamoja na upasuaji wa tumbo (major abdominal surgeries), kuungua kwa moto (burns), ugonjwa wa figo; na kubadilishwa kwa viungo vya mwili kama figo au ini.

Dalili au viashiria vya PUD

Maumivu makali au kiungulia maeneo ya chembe moyo (epigastic pains): Maumivu juu kidogo ya tumbo mara nyingi huendana na muda wa kula chakula.

Mtu mwenye vidonda kwenye tumbo (gastric ulcers) hupata maumivu makali sana kipindi anapokula au mara tu baada ya kumaliza kula wakati aliye na vidonda kwenye sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo hupata maumivu makali anapokuwa na njaa na hupata nafuu pindi anapokula. Dalili nyingine ni kuvimbiwa au tumbo kujaa gesi. Hali hii pia yaweza kuendana na kubeua au kucheua na kuongezeka kwa mate yanayoshuka tumboni baada ya kucheua.

Pia dalili nyingine ni kichefuchefu na kutapika, kupoteza hamu ya kula na kupungua uzito, kutapika damu, kupata haja kubwa ya rangi nyeusi au kahawia yenye harufu mbaya sana. Hii humaanisha mgonjwa anapata haja kubwa au choo kilichochanganyika na damu kwa mbali.

Uwepo wa dalili kama kiungulia cha muda mrefu, kucheua na kutapika baada ya kula na historia ya kutumia dawa za kupunguza maumivu (NSAIDs) kwa muda muda mrefu bila kufuata ushauri wa daktari ni ishara tosha ya kumfanya mgonjwa kumuona daktari kumpima na kumfanyia uchunguzi ili kujiridhisha kuwa hana tatizo la vidonda vya tumbo.

UCHUNGUZI

Vipimo v inav yotumika kat ika kutambua tatizo la vidonda vya tumbo ni pamoja na vipimo vya kuangalia ndani ya utumbo ambavyo ni pamoja na: Kipimo cha Upper GI endoscopy au gastroscopy. Kwa kutumia kipimo hiki, daktari huangalia moja kwa moja ndani ya utumbo wa mgonjwa kuona sehemu iliyo na vidonda pamoja na ukubwa wa tatizo lake.

Aidha vipimo hivi humuwezesha daktari kuchukua sehemu ya utumbo iliyoathiriwa kwa ajili ya kuchunguza zaidi maabara ili kutambua uwepo wa vidonda au tatizo lingine linalomsumbua mgonjwa tofauti na vidonda vya tumbo. Kipimo kingine kijulikanacho kama Barium meal kina uwezo pia wa kuthibitisha uwepo wa ugonjwa wa vidonda vya tumbo.

Comments are closed.