The House of Favourite Newspapers

Fahamu makundi matatu ya ugonjwa wa vidonda vya tumbo

0

urlTUNAENDELEA kuchambua ugonjwa wa vidonda vya tumbo na hii ni sehemu ya mwisho nikiwa na imani kuwa mtafaidika na somo hili. Leo tutazungumzia tiba ya maradhi haya tukimalizia sehemu ya mwisho ya hatua ya ugonjwa huu.

Katika hatua ya mwisho tuliona kuwa wagonjwa wengine hujikuta wakiongezeka mate yanayoshuka tumboni baada ya kucheua au kusikia kichefuchefu na kutapika na kupoteza hamu ya kula na kupungua uzito.

Hali ikiwa mbaya mgonjwa hutapika damu au kupata haja kubwa ya rangi nyeusi au kahawia au kilichochanganyika na damu.

Wenye vidonda vya tumbo wengine wakitumia dawa za kupunguza maumivu bila kufuata ushauri wa daktari watakuwa wanapata kiungulia cha muda mrefu, kucheua na kutapika baada ya kula chakula.

TIBA
Makundi yote hayo ya ugonjwa wa tumbo wanaougua watu watambue kuwa maradhi hayo hutibika.Daktari akigundua mgonjwa ana matatizo haya atatumia dawa mbalimbali za antibiotic kama vile Amoxicillin, Tetracycline, Clarithromycin au Metronidazole au dawa za kupunguza uzalishaji wa tindikali kwa wingi. tumboni.

Wagonjwa wengine hutibiwa kwa kufanyiwa upasuaji hasa wale wanaogundulika kuvuja damu ndani ya mwili kupitia vidonda vya tumbo kwani ugonjwa ukifikia hatua hiyo huweza kusababisha kifo iwapo mgonjwa hatapata tiba haraka.

USHAURI
Si vyema na haishauriwi kabisa mgonjwa kujitibu bila kufuata ushauri wa daktari kwani kwa kufanya hivyo anaweza kupata madhara ikiwa atatumia dawa au dozi isiyostahili.

MAZIWA YA NG’OMBE HAYAPONYESHI
Ipo dhana kwa wagonjwa wa vidonda vya tumbo kuwa maziwa ya ng’ombe yanaponyesha maradhi haya, ukweli ni kuwa hayaponyeshi bali huongeza madhara yatokanayo na ugonjwa huu.

Kitaalam maziwa huwa na tabia ya kutengeneza aina fulani ya kinga au ukuta (protective coat) kwa vimelea vya ugonjwa wa vidonda vya tumbo viitwavyo Helicobacter Pylori ambayo huvikinga vimelea hivi dhidi ya mashambulizi ya dawa na hivyo kufanya dawa kushindwa kuwaua na kuviondoa kabisa vimelea hivyo tumboni.

Ukweli ni kwamba maziwa huondoa tu kwa muda maumivu ya tumbo kwa kupunguza makali ya tindikali iliyopo tumboni lakini baadaye maumivu hurejea na kuwa makali.

Wiki ijayo tutaeleza hatua nne za maradhi haya ya vidonda vya tumbo, ili ujikinge navyo, usikose nakala yako.

Leave A Reply