The House of Favourite Newspapers

Fahamu Sababu Mwili wa Hamza Kuzikwa Usiku

0

MWILI wa Hamza Mohammed aliyefariki dunia katika tukio la majibizano ya risasi kati yake na jeshi la Polisi Jumatano, Agosti 25, 2021 amezikwa Jumapili, Agosti 29, 2021 saa 2:30 usiku katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.

 

Mwili huo umezikwa baada ya kuswaliwa katika Msikiti wa Mamuur uliopo Upanga jijini Dar es Salaam. Awali mwili huo ulitarajiwa kuzikwa saa 7 mchana katika makaburi hayo, lakini msemaji wa familia Abdulrahm Hassan alisema mwili huo ulichelewa kwa sababu ya kazi ya kutoa risasi zilizokwama kwenye mwili wa marehemu.

 

Watu wanne walifariki dunia na sita kujeruhiwa juma lililopita kwenye mapambano ya kurushiana risasi yaliyotokea makutano ya barabara ya Kenyatta na Kinondoni jirani na Ubalozi wa Ufaransa, jijini Dar es Salaam.

 

Tukio hilo lilitokea Agosti 25, 2021 baada ya mtu mmoja ambaye awali hakufahamika kuzua taharuki baada ya kufyatua hewani risasi huku akisikika akisema kuwa anawatafuta polisi.

Leave A Reply