The House of Favourite Newspapers

Fahamu Simu 10 Zinzoongoza kwa Kununuliwa Afrika

0

HAIWEZI kuwa  vigumu kufahamu ni chapa (brand) ipi ya simu ambayo inauza zaidi duniani. Vyanzo tofauti tofauti vinasema chapa za kampuni ya Apple (iPhone) ndio bado zinaongoza katika uuzaji wa simu duniani kote ikifuatiwa na Samsung.

 

Lakini sasa, cha kushangaza simu hizo mbili ambazo ndio zinaongoza kwa mauzo duniani haziuzi sana Barani Afrika. Simu inayoongoza kwa mauzo Afrika ni “TECNO”, na hili ndilo lililofanya watu wengi kubaki midomo wazi.

 

Ukizungumzia orodha ya simu 10 bora zinazouza zaidi duniani chapa (brand), simu za “TECNO” hazipo, lakini bado kwa Afrika ndio chapa (brand) inayongoza kwa kununuliwa.

 

Jambo hili lina utofauti kidogo kwa Afrika kutokana na uwezo wa kipato kwa Wafrika wengi kuwa ni wa hali ya chini, hivyo ndio maana ikawa rahisi kwa chapa (brand) za Kampuni ya “TECNO” kushika nafasi ya 1 Afrika katika masoko.

 

Hii ni kutokana na bei zao kuendana na kipato cha Waafrika wengi  kulinganisha na Simu za Apple na Samsung ambazo zina gharama katika ununuzi wake.

 

Japokuwa Makampuni mengi yaliyumba kiuchumi kutokana na janga la (COVID-19), lakini bado “TECNO” hawakuyumba sana, waliendelea kutengeneza bidhaa kulinganisha na Makampuni mengine na hiyo ni sababu nyingine ya “TECNO” kuwa namba moja Afrika.

 

Hii ndio orodha ya Simu (10) zilizouza sana Afrika kwa mwaka 2020.

 

1) TECNO

2) SAMSUNG

3) ITEL

4) HUAWEI

5) INFINIX

6) XIAOMI

7) OPPO

8) APPLE

9) NOKIA

10) REALME.

 

 

 

Leave A Reply