FAHYMA ACHEKELEA RAYVANNY KUFUNGULIWA

 

Fahyma

MZAZI mwenziye na Mbongo Fleva, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’, Fahyma amefunguka kufurahishwa kwake na kitendo cha baba mtoto wake huyo kusamehewa na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) kwani ishu hiyo ilikuwa inamnyima usingizi.

Akichezesha taya na Risasi Jumamosi, Fahyma alisema katika kitu kilichokuwa kinampa mawazo na kukosa kabisa usingizi ni kufungiwa kwa baba mtoto wake huyo lakini kwa sasa anaishukuru Basata kwa kuwahurumia na kuwafungulia kuendelea na kazi kama kawaida.

“Kufungiwa kwa Rayvanny kulikuwa kunanipa mawazo sana maana nilikuwa nawaza maisha yetu yatakuwaje na tulikuwa hatujui msamaha utatoka lini lakini tunashukuru Mungu wamesamehewa na mwisho wa siku maisha mengine yanaendelea, nitaendelea kumhimiza asirudie kosa tena,” alisema Fahyma.

Rayvanny na Nasibu Abdul ‘Diamond’ walifungiwa na Basata kufanya maonesho yoyote ikiwemo lile la lebo yao la Wasafi Festival lililokuwa likiendelea nchi nzima kwa muda usiojulikana ikiwa ni baada ya kukiuka amri ya baraza hilo la kutoimba Wimbo wa Mwanza, walikiuka na kuuimba jukwaani lakini Jumanne iliyopita wamesamehewa na kufutiwa adhabu hiyo.

Toa comment