The House of Favourite Newspapers

Hizi Hapa Faida saba za Tango Mwilini Mwako

tango.jpeg

HAWANA makosa wale waliosema kuwa mboga za majani na matunda ni kinga kwa afya yako. Matunda mengi yana manufaa lakini tango linaonekana kutia for a kwa manufaa katika mwili wa binadamu. Tango ni aina ya tunda jamii ya tikitimaji kwani lina maji mengi lakini sio tamu kama tikiti.

Tango linasifika kwa kuwa na vitamin zote unazohitajimwilini  kwa siku kwani moja tu lina vitamin B1, B2, B3, B4 na B6, madini ya chuma, potasium na zinc. Pili, unapojisikia kuchoka mchana, kula tango moja ambalo linaweza kukupa nguvu kwa saa kadhaa.

Tatu, ngozi yako inahitaji tango kutoa seli zilizokufa na makunyanzi. Weka au sugulia vipande vya tango usoni au sehemu iliyoathirika kila siku na utaona maajabu baada ya siku chache. Nne, kama unataka kuondoa uchovu hasa wa pombe (hangover)  au maumivu makali ya kichwa, kula tango ukiongoza

sukari (kama huna kisukari), vitamin utakazopata zitaweka mambo sawa mwilini. Tano, kama umemaliza kula, unahisi una harufu mbaya mdomoni nyakati za mchana. Tafuna vipande vya tango na utapata harufu nzuri ya mdomo. Sita, kama midomo imekauka na inauma? Chukua kipande

cha tango na sugulia mdomoni, utaona mabadiliko katika midomo yako. Saba, kama umekosa muda wa kula mchana, kula tango moja bila kumenya maganda na litaweza kukaa tumboni kwa saa zaidi ya nane. Kutokana na faida hizo, unashauriwa kula tango kila siku, utaona manufaa yake.

Comments are closed.