The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Aipongeza Taifa Stars licha ya kichapo cha 3-0 dhidi ya Morocco

0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amezungumza na wachezaji wa timu ya Taifa ya mpira wa miguu Taifa Stars jioni hii kwa njia ya simu na kuwapa moyo kuelekea mchezo wao wa leo na timu ya Taifa ya Morocco ikiwa ni mechi yao ya kwanza katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Afcon 2023 yanayofanyika nchini Ivory Coast. Rais Samia amezungumza na timu hiyo ya Taifa akiwa visiwani Zanzibar tarehe 17 Januari, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameipongeza Taifa Stars licha ya kichapo cha 3-0 dhidi ya Morocco huku akibainisha kuwa mchezo ulikuwa mzuri lakini bahati haikuwa upande wa Stars.

“Mchezo mzuri usiku wa leo vijana wetu Taifa Stars japo bahati haikuwa upande wetu. Tunaendelea kuwatakia kila la kheri na Taifa liko nyuma yenu katika mechi zenu zinazofuata,” ameandika Dkt. Samia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii.

Leave A Reply