The House of Favourite Newspapers

FAMILIA YA KIBA; MIEZI 3, NDOA 3

Ali Saleh Kiba na Mkewe 

IKIWA zimebaki siku saba kufikia ndoa ya mwanadada Zabibu kiba ambaye ni dada wa mkali wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba, siri ya kufululiza kwa ndoa hizo yajulikana.

Mnamo mwaka jana gazeti hili liliweza kuzungumza na Mama Kiba juu ya suala la ndoa na kusema anatamani sana watoto wake waoe na binti yake aolewe na anaomba Mungu amjibu maombi yake. Alisema atafurahi sana hiyo siku ikifika kwa sababu watoto wake washakuwa watu wazima na amechoshwa na maneno ya watu dhidi ya watoto wake.

Kama wanavyosema Mungu huwa hawahi wala hachelewi, maombi ya Mama huyu yalianza kujibiwa; ulianza kusikika uvumi katika mitandao ya kijamii kwamba, Ali Kiba anataka kuoa; wengi waliamini ni utani na mambo ya kutafuta kiki tu

ALIKIBA ILIKUAJE?

Zilianza kusikika tetesi kuwa Ali Kiba anaoa lakini haikujulikana kwa haraka kuwa anamuoa nani kwa sababu maandalizi ya ndoa yalifanywa kwa siri mno. Wapo waliohisi atamuoa mwanadada Jokate Mwegelo, lakini ‘mshale’ haukulenga shabaha, hisia hizo hazikuwa sawa.

Hayawihayawi yakawa. Aprili 19, mwaka huu mjini Mombasa Kenya, Ali Kiba akafunga ndoa na mwanadada Aminah Rikesh. Sherehe ya kwanza ilifanyika Mombasa na funga kazi yake ikafanyika Dar huku ikirushwa Live kupitia AzamTv. Ilikuwa ni Harusi ya aina yake ilihudhuliwa na watu mashughuli, huko Mombasa Gavana wa jimbo hilo, Hassan Joho alikuwa miongoni mwa waalikwa wakati hapa Tanzania Mke wa Rais Mstaafu, Mama Salma Kikwete alikuwa mwalikwa mahsusi.

Kwa muonekano sherehe hiyo ilimpa heshima Mama Kiba ambaye wakati wote alionekana kutabasamu kama mtu mwenye kauli moyoni kwamba: “Ndoto za furaha yangu leo zimetimia.” Kuna msemo wa: ‘safari moja huanzisha nyingine’, Ali Kiba alikuwa kama kawafungulia wenziye njia ya neema, mdogo wake Abdul Kiba alifuata nyayo, tena yeye hakutaka kusubiri saanaaa!Picha inayohusiana

ABDUL KIBA NAYE NDOA

Kama masihala Abdul naye alichukua jiko jumla kwa kumuoa Bibiye Ruwayda na kumuweka ndani April 22 mwaka huu ikiwa zimepita siku kama tatu hivi tangu kaka yake Ali afunge ndoa. Harusi ya kijana huyo ilifanyika Nyumbani kwao Kariakoo, Dar es salaam, pia walifanya sherehe ya pamoja yeye na kaka yake Ali kiba, ikiwa kama kuwatambulisha wake zao mbele ya mashabiki wao; si utani ilinoga sana.

Tukio hilo la kheri pia liliongeza furaha kwa Mama Kiba, watu wengi walimmwagia sifa zake kuwa anajua kulea katika misingi ambayo ni mizuri ya kumjua Mungu na ndiyo maana watoto wake hawana skendo zisizo na maana.Tokeo la picha la zabibu kiba

ZABIBU NAYE HUYOOO

Wiki iliyopita zilianza kusambaa picha zikimuonesha akiwa katika mavazi ya harusi na kuzua viulizo vingi kuwa huenda naye keshaolewa na msakata ndinga Abdul Banda, lakini hakuna aliyepata jibu sahihi. Ndipo gazeti hili lilipoamua kumtafuta Zabibu na kuzungumza naye ambapo alisema ni kweli anataka kuolewa lakini picha zinazosambaa si za harusi bali ni maandalizi tu ya kuelekea kwenye ndoa inayotarajiwa kufungwa Agosti

1, MWAKA HUU.

Basi kama hilo nalo liko mbioni wadau tunawaombea heri Mwenyezi Mungu awape furaha waliyokuwa wakiitafuta, CIAO.

Stori: Shamuma Awadhi

Comments are closed.